PITA PITA ZANGU NDANI YA MKOA WA LINDI, LEO TUMEANGAZIA JIMBO LA MTAMA KIJIJI CHA CHIHUTA

Hii ni zahanati ya chihuta na nyumba ya Daktari ilijongwa tangu mwaka 1973 katika kijiji cha Chihuta kata ya Mandwanga Wilaya ya Lindi Vijijini Mkoa wa Lindi. 
Nyumba ya Daktari Zahanati ya Chihuta

Jengo la zahanati linakabiliwa na changamoto ya chumba cha kujifungulia akina mama wajawazito maana inafikia kipindi wakina mama wanajifungulia chini, pia inakkabiliwa na Upungufu wa wahudumu wa Afya kwani hivi sasa ina muhudumu mmoja anayefanya kazi zaidi ya masaa ishirini na nne na anakaa nyumba ambayo haina ukarabati wowote.

Hali iliyofikia nyumba hiyo haistahili kuishi mwanadamu, Serekali Inaombwa kuiangalia zahanati hii pamoja na makazi ya Mtuahuduma huyu, hii inaweza kutoa morali ya kazi kwa wahudumu wa afya kufurahia kufanya kazi katika kijiji hicho kwa asilimia 100.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post