Unknown Unknown Author
Title: NAY WA MITEGO AJA NA COLLABO MBILI ZA KIMATAIFA, NI KUTOKA NIGERIA NA GHANA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rapper Nay wa Mitego amesema ameamua kwenda kimataifa zaidi ambapo mpaka sasa ameshafanya kolabo mbili za wasanii nje Nay amesema yakuwa...
Rapper Nay wa Mitego amesema ameamua kwenda kimataifa zaidi ambapo mpaka sasa ameshafanya kolabo mbili za wasanii nje
Nay amesema yakuwa amepokea maoni kutoka wadau mbalimbali kuhusu kupandisha muziki wake thamani.“Unajua msanii anatakiwa akue kama unavyoona vitu vingine ambavyo vinakuwa,” amesema Nay.

“Mwaka huu nimeanza kupandisha bei zangu za show, for this time nimebadilisha vitu vingi, show zitakuwa tofauti ambavyo nilikuwa nikifanya mwaka uliopita. Nimepokea maoni mengi sana kuhusu wimbo wangu wa Akadumba, umefanya poa sana. Sasa kama ninafanya muziki mzuri kwanini na mimi nisiwe mkubwa zaidi?

Wengi wanasema ‘nenda international’, wengine ‘fanya video na Godfather nyumbani inatosha’ Kwa mikakati ambayo nimeipanga, kolabo mbili zipo tayari. Ngoma mbili zipo tayari, moja nimefanya na msanii wa Nigeria na nyingine wa Ghana na zipo mwishoni kukamilika,”
ameongeza rapper huyo.

“Pia nipo tayari kufanya kolabo na msanii yoyote wa nje ili kusukuma muziki wangu mbali zaidi na kuitangaza nchi yangu. Kwahiyo nafikiria watu wategemee ngoma moja kwangu peke yangu na baada ya hapo wategemee kolabo kubwa kutoka nje ya Afrika Mashariki. Na nina imani itanipeleka sehemu nyingine pia.”

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top