MOSES IYOBO AFUNGUKU KUHUSU MIMBA YA AUNT EZEKIEL, ASEMA MIMBA HIYO NDIO FARAJA YAKE

Dansa mahiri wa staa wa muziki Bongo na nje ya nchi, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye Moses Iyobo, amefunguka kuwa hakuna kitu kinachompa faraja kubwa kama mimba ya mpenzi wake ambaye ni mwigizaji wa filamu, Aunty Ezekiel.
Moses Iyobo na Aunty Ezekiel
Akizungumzia ujauzito wa mpenzi wake, Iyobo ambaye nyuma kidogo alipost picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kutoa pongezi kwa mpenzi wake huyo kwa kumbebea ujauzito, alisema kuwa hakuna kitu ambacho anaona fahari kama hicho.

“Mimi tu nikiwaza mtu ambaye ninampenda kwa dhati ana mimba yangu napata faraja kubwa sana hivyo kila siku namuomba Mungu ajifungue salama na ampitishe katika majaribu mazito,” alisema Iyobo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post