Unknown Unknown Author
Title: MARKET FC VINARA WA LIGI DARAJA LA TATU MKOA WA LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi cha Kwanza cha Market Fc kilichocheza dhidi ya Timu ya Beach Boys Leo hii Kinachofundishwa na Newton Kumpanga, Katika Ligi Daraja...
Kikosi cha Kwanza cha Market Fc kilichocheza dhidi ya Timu ya Beach Boys Leo hii Kinachofundishwa na Newton Kumpanga, Katika Ligi Daraja la Tatu Mkoa wa Lindi katika Uwanja wa Ilulu
Kikosi cha Kwanza cha Beach Boys kilichocheza dhidi ya Timu ya Market Fc Leo hii Kinachofundishwa na Kocha Abdallah Malinda (mchezaji wa zamani wa Kariakoo Fc) katika Ligi daraja la Tatu Mkoa wa Lindi katika Uwanja wa Ilulu
Na. Ahmeid Abdullaziz - Lindi
Ligi Daraja la Tatu Mkoani Lindi limefikia Patamu Baada ya Leo Timu za Beach Boys na Market Fc kutoka Droo ya Magoli 2 - 2 katika Uwanja wa Ilulu - Lindi.

Timu ya Market Fc Ndio iliyokuwa ya Kwanza Kufungua kalamu ya Magoli katika Mechi hiyo iliyoshuhudiwa na Mashabiki lukuki wa Mkoa wa Lindi kwa kupitia Mchezaji wake Nonda Shabani mnamo dakika ya 6 ya Kipindi cha Kwanza mara baada ya kupiga Shuti kali lililomshinda Mlinda mlango wa Beach Boys kudaka wala kulipangua ijapokuwa alijitahidi kuruka sana na Kutinga Nyavuni, 

Mpira ulikuwa Mkali sana Hasa ikionekana Timu ya Beach Boys wanasaka Point Tatu muhimu ili waweze kuwa Vinara wa Ligi hiyo kutokana na Kujinyakulia Point 2 katika Mechi za awali, Kupitia kwa Mshambuliaji wake Machachari Idrisa, Beach Boys ilipata Bao la Kusawazisha kupitia Mkwaju wa Penalt mnamo dakika ya 13 ya Mchezo huo. 
Hadi Timu hizo zinaenda mapumziko zilikuwa zimetoshananguvu 1-1.

Kipindi cha Pili kilianza kwa Kasi kwa timu zote mbili kushambuliana kwa  zamu na Timu ya Market Fc ndio ilikuwa ya Kwanza kupata mafanikio ya Mashambulizi yake langoni mwa Beach Boys kupitia Mchezaji wake Rajabu Msela katika dakika ya 76 na kufanya matokeo kubadilika na kuifanya timu hiyo kuwa ndio Timu Inayoongoza Ligi hiyo.
Lakini Mwamuzi wa Mchezo huo aliweza kuzima matumaini ya Timu ya Market Fc kwa kuwazawadia Timu ya Beach Boys Penalt ya pili mnamo dakika ya 84, kwa kosa la beki wa Market Fc Mpira kugonga katika Mkono wake katika eneo la hatari na ni Idris tena aliepiga Penalt hiyo na Kumchamvua Golkipa wa Market na kuiandikia Timu yake Goli la kusawazisha. 
Shujaa...: Idris akishangilia Mara baada ya Kuisawazishia Timu yake Bao la Pili lililotokana na Penalt katika kipindi cha Pili cha Mchezo huo

Hadi Mwiisho wa mchezo huo Beach Boys 2 - 2 Market Fc 

Kwa matokeo hayo Timu ya Market Fc bado inaongooza Ligi hiyo kwa Jumla ya Point 5 huku ikifuatiwa na Beach Boys yenye point 3, Timu za Stand Worious na Kusini Soccer zote kwa Pamoja zina Point 2 huku Time ya Maafande wa Magereza wakiburuza Mkia kwa kuwa na Point 1.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top