Unknown Unknown Author
Title: JAMBAZI ANUSURIKA KUUWAWA DARAJANI ZANZIBAR HII LEO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Watuhumiwa wawili katika tukio la ujambazi lililotokea Mchana wa leo eneo la Darajani Jua Kali,Zanzibar wametiwa mbaroni baada ya kuzidiw...
Jambazi

Watuhumiwa wawili katika tukio la ujambazi lililotokea Mchana wa leo eneo la Darajani Jua Kali,Zanzibar wametiwa mbaroni baada ya kuzidiwa nguvu na wananchi wenye wakati walipokuwa wakiwakimbia Polisi.

Inadaiwa kuwa watuhumiwa hao walikuwa watatu na walitaka kuiba katika maduka na mawakala wa huduma za pesa yaliyopo eneo la Mnazi Mmoja. Baada ya kushtukiwa walikimbia na kufukuzana na Polisi hadi katika maeneo ya Darajani ndipo wananchi kwa kushirikiana na polisi wakawadhibiti na kuwakamata. Hata hivyo mmoja wao alifanikiwa kutoroka na hadi sasa anasakwa na jeshi la polisi.

Pia wapo baadhi ya wananchi wamelazwa hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kupatwa na mshtuko kutokana na risasi zilizokuwa zikipigwa hewani na mmoja aligongwa na gari la watuhumiwa hao wakati wa kukimbizana na askari.
Mmoja kati ya waliokamatwa na aliepata kipigo kikali anadaiwa kuwa ni jambazi sugu ambae alikuwa akitafutwa na Polisi kwa kipindi kirefu.

Watuhumiwa hao walikuwa na gari aina ya Toyota Noah lenye namba za Usajili T 736 CGT na walikamatwa baada ya gari lao hilo kushindwa kuendelea na safari baada ya kuingia kwenye njia ambayo hairuhusiwi.

JambaziAskari Polisi pamoja na raia waliokuwepo eneo la tukio wakiwa wamemzunguka mmoja wa watuhumiwa hao wa ujambazi baada ya kumtia mbaroni mchana wa leo,katika eneo la darajani Jua Kali,Zanzibar.
Jambazimmoja wa watuhumiwa hao akiwa chini ya ulinzi ndani ya Gari la polisi.
JambaziMtuhumiwa mwingine ndani ya Gari.
Jambazi
Hii ndio gari waliyokuwa wakiitumia Watuhumiwa hao.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top