Unknown Unknown Author
Title: HICHI NDICHO KILICHOTOKEA BUNGENI MAPEMA LEO ASUBUHI NA KUSABABISHA SPIKA KUAHIRISHA SHUGHULI ZA BUNGE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mbatia alisimama na kutoa hoja ya dharura ijadiliwe Bungeni kuhusu Polisi Dar es Salaam kutumia nguvu dhidi ya wanachama wa CUF na kuwa...


Mbatia alisimama na kutoa hoja ya dharura ijadiliwe Bungeni kuhusu Polisi Dar es Salaam kutumia nguvu dhidi ya wanachama wa CUF na kuwapiga.

Mbatia: "Nimesikitishwa sana, Lipumba amepigwa, watoto wamepigwa, waandishi wa habari wamepigwa, na Polisi wakasema wamepewa maagizo"

Mbatia: "Prof Lipumba ni Mwenyekiti wa chama chenye wabunge zaidi ya 30 na Mwenyekiti wa chama kinachoshiriki serikali ya Zanzibar, sasa kama yeye anafanyiwa hivi itakuwaje Wananchi wa kawaida?"

Mbatia: "Naomba kutoa hoja Bunge liahirishe shughuli zake ili tujadili tatizo hili lililotokea"


Lakini Spika Anna Makinda aliipinga hoja yake na kusema,

Spika Makinda: "Naiagiza serikali iandae taarifa kamili, kesho ilete humu Bungeni, ndipo nitaruhusu hoja hii ijadiliwe, Sasa Hapana".

Spika Makinda: "Someni kanuni vizuri, zinaniruhusu kuamua kama kadri ninavyoona, hoja za namna hii haziungwi mkono"

Hilo likazua tatizo baada ya Baadhi ya wabunge wengi wa upinzani kugoma kuendelea na ratiba, Huku wakitaka ijadiliwe, walianza kupiga kelele.
Spika Makinda akaamua kusitisha shughuli za Bunge hadi saa 10:00 jioni kutoa nafasi ya makubaliano kuhusiana na suala hilo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top