Unknown Unknown Author
Title: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LATANGAZWA, WAAPISHWA LEO HII
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akizungumza na vyombo vya habari jioni hii wakati akitangaza mabadiliko madogo ya  Baraza la M...
Ombeni Sefue
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akizungumza na vyombo vya habari jioni hii wakati akitangaza mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri,Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo ametangaza mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri,ambalo Ameliapisha jioni hii Ikulu,Jijini Dar es Salaam.

Akitangaza uteuzi huo muda mchache kabla ya Mawaziri hao kuapishwa, Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue amesema uteuzi huo unahusu pia kujaza nafasi mbili zilizoachwa wazi na Profesa Anna Tibaijuka Na Profesa Sospeter Muhongo.

Profesa Tibaijuka, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alieachishwa kazi kutokana na kuhusika kwake katika sakata la akaunyti ya Tegeta Escrow.
Kwa upande wa Profesa Muhongo aliachia ngazi mwenyewe mapema leo,  kwa kile alichotaja kuipisha Serikali iendelee kuwatumikia Wananchi badala ya kuendelea na malumbano ya Escrow.

Katika mabadiliko hayo,sura mpya za manaibu mawaziri zimeingia na baadhi ya mawaziri wamehamishwa wizara.

Akitangaza Mabadiliko hayo,Balozi Sefue aliwataja mawaziri hao kama ifuatavyo.

MAWAZIRI
1. Mh. George Simbachawene - Waziri wa Nishati na Madini2. Mh. Mary Nagu - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mahusiano na Uratibu)3.Mh. Christopher Chiza - Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji4. Mh. Harrison Mwakyembe - Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki5.Mh. William Lukuvi - Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi6.Mh. Steven Wasira - Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika7.Mh. Samwel Sitta -Waziri wa Uchukuzi8.Mh. Jenista Muhagama - Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge

MANAIBU WAZIRI1. Stephen Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais - Muungano2. Mh. Angela Kairuki -  Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi3. Mh. Ummy Mwalimu - Naibu Waziri wa Katiba na Sheria4. Mh. Anna Kilango - Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi5 . Mh. Charles Mwijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini

WATEULE WANAAPISHWA HIVI SASA NA RAIS KIKWETE ..

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top