Unknown Unknown Author
Title: UBABAISHAJI WA LIREFA, VILABU 5 VYAJITOA KUSHIRIKI LIGI DARAJA LA TATU MKOANI LINDI,
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
UMOJA WA VILABU MANISPAA YA LINDI WAKIWA KATIKA KIKAO, LEO HII Ligi Daraja la Tatu lililotegemewa kuanza Kutimua Vumbi Ndani ya Mani...
Umoja wa Vilabu Manispaa ya Lindi
UMOJA WA VILABU MANISPAA YA LINDI WAKIWA KATIKA KIKAO, LEO HII

Ligi Daraja la Tatu lililotegemewa kuanza Kutimua Vumbi Ndani ya Manispaa ya Lindi Leo hii limeingia Dosari ya aina yake kwa Vilabu Shiriki kuamua Kujitoa katika Ligi hiyo Kutokana na Kile kilichozungumzwa kuwa ni Ubabaishaji wa Mamlaka Husika inayotakiwa kuendesha mashindano hayo kwa kuahirisha mara kwa mara Mashindano hayo kitu ambacho kina wapa wakati mgumu vilabu hivyo katika Uendeshaji wa Timu.

Umoja wa Vilabu Manispaa ya Lindi
Akizungumza na Lindiyetu.com Mwenyekiti wa Kikao kilichofanyika leo hii cha Umoja wa Vilabu hivyo Ndg RAJABU BAKARI Amesema kuwa wamefikia uamuzi huo wa kujitoa katika mashindano hayo kutokana na Ubabaishaji wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Lindi, Kwa kushindwa kuendesha mashindano hayo kwa wakati muafaka na kufanya vilabu hivyo kuingia katika wakati mgumu wa kiuchumi wa kuwahudumia wachezaji. 

Pia Mwenyekiti aliongeza kuwa wameadhimia Kumuondoa/Kumvua Mwenyekiti wa Chama cha Mpira ambae pia ni Mwenyekiti wa Vilabu vya Manispaa ya Lindi Ndg Francis Ndulane kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ya Uenyekiti katika Umoja huo.
Umoja wa Vilabu Manispaa ya Lindi
Katika hali isiyo ya kawaida wadau hao wamelalamikia uendeshwaji wa Chama hicho kuwa haufuati taratibu za Kisheria kwani hata taarifa za Ubadilishwaji wa Tarehe za Kuanza Ligi hiyo ilitumwa kwa Njia ya Simu badala ya Barua maalumu kwa Vilabu shiriki na pia alie tuma ujumbe huo si Muhusika wa Kazi hiyo.
Umoja wa Vilabu Manispaa ya Lindi
Vilabu vilivyo shiriki katika kikao hicho cha leo hii ambavyo vimadhamiria kujitoa katika ligi hiyo ni :-
  1. Market Place fc
  2. Beach Boys
  3. Kusini Soccer
  4. Stand Worious
  5. Magereza FC
Vilabu Shiriki jumla vilikuwa 7 ambavyo vilivyo baki ni BAFANA BAFANA na NYANGAO FC

Mtandao huu ulifanya jitihada za Kumtafuta afisa Habari wa Lirefa kwa Njia ya simu kuzungumzia sakata hili lakini hakuweza kupatikana Hadi tunaingia mitamboni, Endelea kuwa nasi tutazidi kumtafuta iliaweze kuweka bayana nini hasa upelekwaji mbele wa Mashindano haya.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top