Unknown Unknown Author
Title: #SIMANZI :: ALIYESHINDA UCHAGUZI TIKETI YA CHADEMA AKUTWA AMEKUFA KISIMANI HUKO GEITA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wananchi wa mtaa Msalala road wakiangalia shimo ambalo limesababisha kifo cha mgombea wao Bertha Chimanyi usiku wa kuamkia leo Ber...
Wananchi wa mtaa Msalala road wakiangalia shimo ambalo limesababisha kifo cha mgombea wao Bertha Chimanyi usiku wa kuamkia leo
Bertha Chimanyi enzi za uhai wake


Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita
Kumetokea sintofahamu ama kwa lugha nyingine hali isiyo ya kawaida iliyowastua wananchi wa mtaa wa Msalala Road mkoani Geita ,ya kuondokewa na mgombea wa nafasi ya wajumbe wa serikali za mitaa viti maalumu kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bertha Nchimanyi (40) baada ya kukutwa amekufa kisimani.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 9:00 wakati mgombea huyo alipotoka nje kuongea na simu yake ya mkononi.
Inaelezwa kuwa marehemu alikuwa akisimamia zoezi la kuhesabu kura zake,na wakati zoezi hilo likiendelea alitoka nje kuongea na simu na hakurudi tena.
"Martha nilikuwa naye ilipofika majira ya saa 9 usiku wakati tunahesabu kura ,aliniambia anatoka mara moja nje lakini hakurudi tena"  aliiambia Malunde1 blog, mgombea wa nafasi ya mwenyekiti kupitia Chadema Elineema Mafie.

Naye wakala wa mgombea huyo Maselina Simbasana ambae alisaini matokeo ya marehemu huyo baada ya kuonekana hayupo, alisema marehemu alikuwa na mtoto mdogo hivyo walivyomtafuta walidhani huenda alikwenda nyumbani kunyonyesha mtoto wake.

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Geita Joseph Konyo alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema: na kwamba, jeshi linaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini chazo cha tukio.
“Ni kweli kuna tukio la mgombea wa chadema kutumbukia kisimani, kwa taarifa tulizonazo inaelezwa alitoka nje kuongea na simu wakati anaongea hakujua kama kuna kisima kirefu eneo alilokuwepo, alitumbukia na kufariki dunia”.

Katibu wa Chadema Jimbo la Geita Mutta Robert alisema kuwa kifo cha mgombea huyo ni Mapenzi ya Mungu .
“Mgombea wetu ameondoka na alikuwa ameshinda ,alikuwa mchapakazi mzuri ,tulimpenda zaidi lakini Mungu amempenda zaidi na yote tunamwachia yeye”alisema Robert.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top