Unknown Unknown Author
Title: UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA:: MCHUANO MKALI KATI YA CCM NA CHADEMA UWENYEVITI WA MTAA MKOA WA ARUSHA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wapiga kura sehemu mbalimbali Chama cha mapinduzi kimeweza kuibuka kidedea katika uchaguzi wa uwenyekiti wa mitaa katika mitaa yote i...
Uchaguzi wa serikali za mitaa
Wapiga kura sehemu mbalimbali

Chama cha mapinduzi kimeweza kuibuka kidedea katika uchaguzi wa uwenyekiti wa mitaa katika mitaa yote iliopo ndani ya mkoa wa Arusha baada ya kuvishinda vyama vingine vya upinzani .

Akitangaza matokeo ya uwenyeviti wa mitaa mkurugenzi wa jiji la Arusha Iddi Juma alisema kuwa mpaka sasa uchaguzi wa uwenyekiti umekamilika katika mitaa yote na vituo vyote isipokuwa kituo kimoja ambacho uchaguzi wake utarudiwa siku ya kesho.

Alisema kuwa katika uchaguzi huu jumla ya wananchi 1,13909 walijiandikisha kupiga kura na jumla ya vyama sita vilisimamisha wagombea katika kila mtaa ambapo alitaja vyama ambavyo vilisimamisha wagombea kuwa ni pamoja na ACT,chama cha mapinduzi CCM,NCCR mageuzi ,CUF pamoja na TLP .

Akitaja matokeo ya uwenyekiti wa mitaa alisema kuwa ccm imeweza kuongoza kwa kupata mitaa mingi zaidi ambapo alisema kuwa CCM imeweza kupata kura 78 ambapo kati ya kura hizo kura sita ni za kupita bila kupigwa, ikifuatiwa na chadema ambao wana kura 75 ,ACT ikiwa aijapata kura, NCCR ikiwa aijapata kura, CUF ikiwa aijapata kura pamoja na TLP 
Uchaguzi wa serikali za mitaa
Aidha alibainisha kuwa jumla ya vituo 154 vilikuwa wepo kwa ajili ya kupigia kura na vyote vimekamilisha uchaguzi isipokuwa kimoja ambapo kilifutiwa matokeo hayo na kulazimika kurudiwa ambapo alisema kuwa katika kituo hicho uchaguzi utarudiwa hapo kesho.

"Mpaka sasa uchaguzi wa uwenyekiti umemalizika ila tumelazimika kurudia uchaguzi katika vituo vitatu ambapo katika vituo hicho kituo kimoja ambacho ni cha Oysterbay uchaguzi utarudiwa kwa watu wote na maanisha uchaguzi wa kuanzia kwa mwenyekiti wa mtaa ,wajumbe watano pamoja na wajumbe watatu wa viti maalumu huku katika kituo cha AICC -Sekei uchaguzi utarudiwa kwa wajumbe watatu wa viti maalumu ambapo hii inatokana na kura za kufungana kwani wote walipata 31 kwa 31 na katika kituo cha Oldpolisi line ambapo napo uchaguzi utarudiwa kwa watu wawili ambao nao pia ni wajummbe wa viti waamaalu walifungana kwa kura 64 kwa 64".

Juma alisema katika uchaguzi wa kesho ambao wanarudia wamejipanga vizuri kusimamia kwani nguvu zote wanazielekeza katika vituo hivyo ambapo alibainisha kuwa katika kila kituo kutakuwa na wasimamizi nane pamoja na ulinzi wa kutosha.

Aidha alitumia fursa hii kuwashukuru wananchi wate na viongozi kwa kufanya uchaguzi wa amani na kistarabu pamoja na kuvumiliana huku akiongeza kuwa namatumaini utulivu huu na uvumilivu walionyesha utaendelea hata katika vituo hivi ambavyo vinarudiwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top