Unknown Unknown Author
Title: KLOP AKIRI KUWA NA KAZI NGUMU KUVUKA 16 BORA DHIDI YA JUVENTUS
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya shirikisho la soka barani Ulaya kukamilisha mpango wakupanga ratiba ya hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya mabingwa barani h...
KLOP
Baada ya shirikisho la soka barani Ulaya kukamilisha mpango wakupanga ratiba ya hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya mabingwa barani humo, meneja wa klabu ya Borussia Dortmund Jurgen Klopp amekiri kuwa na mlima mrefu wa kupanda mbele ya mabingwa wa soka nchini Italia Juventus.

Wawili hao wamepangwa kukutana katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ikiwa ni mara ya kwanza kutokea tangu walipochuana katika mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 1997 uliochezwa katika uwanja wa Olympic huko mjini Munich nchini Ujerumani.

Klopp amesema ni vizuri kupangwa na klabu nguli kama Juventus, lakini amekiri wazi kwamba klabu hiyo kwa sasa ipo katika kiwango cha hali ya juu hivyo itamlazimu kufanya kazi ya ziada kukiandaa kikosi chake.

Amesema katika soka lolote laweza kutokea na hatua ya kuanza kuchukua tahadhari kwake anaibeba kama sehemu ya kuanza maandalizi mapema kuelekea katika mtanange huo ambao utaunguruma Februari 24 mwaka 2015.

Hata hivyo Borussia Dortmund wamekua na rekodi nzuri kwa kufanya vyema katika michezo ya hatua ya 16 bora kwa kipindi cha miaka minne mfululizo tangu mwaka 2010.

Mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano utakaochezwa Februari 2015 utachezwa mjini Turine nchini Italia na kisha mchezo wa pili utapigwa mjini Dortmund nchini Ujerumani March 18.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top