Unknown Unknown Author
Title: ILULU SACCOS YACHANGIA SARUJI UJENZI WA MAABARA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Chama cha akiba na mikopo cha Ilulu(ILULU SACCOS) cha Lindi katika manispaa ya Lindi kimeunga mkono juhudi serikali katika ujenzi wa maab...
Chama cha akiba na mikopo cha Ilulu(ILULU SACCOS) cha Lindi katika manispaa ya Lindi kimeunga mkono juhudi serikali katika ujenzi wa maabara katika shule za sekondari kwa kuchangia mifuko 20 ya saruji. 

Akikabidhi mchango wa saruji hiyo yenye thamani ya shilingi 320,000/= kwa mkuu wa wilaya ya Lindi, Dkt Nassoro Himidi, Mwenyekiti wa chama hicho Ahmad Namwadilanga. Alisema chama hicho kimechangia saruji hiyo kutokana na kuamini kwamba mpango huo unafaida kubwa katika sekta ya Elimu hasa katika somo la sayansi ambalo ni muhimu kwa karne hii ya sayansi na teknolojia.
Alisema ni vigumu nchi kupata maendeleo kwa kasi kubwa iwapo tatizo upungufu wa wataalam wanaotokana na masomo sayansi halitaondolewa.Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba hatua ya kwanza ambayo nimuhimu katika kujenga uelewa wawanafunzi katika masomo hayo ni shule kuwa na maabara ambazo zitatumika kujifunza kwa vitendo.

Alisema kwakuwa taasisi hiyo niyakijamii na shule za sekondari zinazojengwa maabara ni za wananchi.Chama chake kimegawa sehemu ya faida inayotokana na biashara inayofanywa na chama hicho ili kuchangia ujenzi huo.
Kwa upande wake dkt ambaye alipokea saruji hiyo itakayotumika kwa ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari ya Angaza.Alisema wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwamo mashirika na taasisi zisizo za kiserikali wilayani humo kuiunga mkono serikali katika mpango huo kwa kuchangia vifaa vya ujenzi na fedha."ujenzi wa maabara unafaida kubwa sana kwani kama mnavyojua katika mikoa ya Lindi na Mtwara imegunduliwa gesi,watalaam wengi watakao hitajika kwenye viwanda na maeneo mengine ya sekta nishati niwalitokana na masomo ya sayansi"alisema dkt Himidi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top