Unknown Unknown Author
Title: KANISA LATAKA WALIOSHIRIKI KUCHOTA FEDHA KWENYE AKAUNTI YA ESCROW WAFIKISHWE KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na.A hmeid Aziz Serikali imeombwa kuwachukilia hatua kali watakaobainika kupanga, kushiriki na kuchota fedha za akaunti maalum ya Tegeta...
ESCROW
Na.Ahmeid Aziz
Serikali imeombwa kuwachukilia hatua kali watakaobainika kupanga, kushiriki na kuchota fedha za akaunti maalum ya Tegeta ESCROW bila kumpendelea au kumuonea mtu.

Wito huo ulitolewa mwanzoni mwa wiki hii na mkuu wa jimbo la kasikazini magharibi,mchungaji Charless Mtweve kwenye ibada iliyofanyika mjini Nachingwea. Mtweve ilikurejesha imani ya wananchi kwa serikali watakaobainika kuhusika katika kashifa hiyo ambayo inaweza kuweza kuathiri mpango wa usambazaji umeme vijijini wafikishwe kwenye vyombo vya sheria bila kumpendelea au kumuonea mtu. 

Alisema rais anatakiwa kutumia busara na hekima kubwa itayoambatana na utulivu katika kutekeleza ushauri na mapendekezo ya bunge kuhusiana na sakata hilo ili watakaositahili kuvuliwa nyazifa zao wavuliwe kwa haki baada ya yeye kujidhirisha.

Alisema suala hilo nizito kwani linatishia kwakukwamisha mipango mbalimbali ya serikali ikiwamo mpango wakusambaza umeme vijijini. Hivyo busara,hekima na utulivu vinahitajika sana katika kulishugulikia na kulitolea maamuzi. Alibainisha kuwa kutokana na uzito wa suala hilo wananchi hawana budi kumpa nafasi rais kupitia mapendekezo na ushauri wa bunge kwa utulivu badala ya kumtaka atoe uamuzi haraka kabla ya kujiridhisha.

Mchungaji huyo alitoa wito kwa watu waliopewa dhamana ya uongozi na utawala kutumia vema dhamana hizo kwa kuwa waadilifu badala ya kuzitumia kwa maslahi yao binafsi. Alisema kupungua kwa imani kunasababisha tamaa kwa viongozi ikiwamo wadini ambao walitakiwa kuwa mfano wa uadilifu wamegeuka na kuwa wezi katika maeneo wanayoyaongoza.
"watu wanaotenda maovu hawatafakari njia zao wamejawa na kiburi kinachosababisha wajione kuwa wao ni wao." alisema Mtweve.

Ibada hiyo ilitumika pia kumshukuru Mungu kwa kumponya rais Kikwete kutokana na upasuaji aliofanyiwa na kurudi salama nchini.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top