PATA KUJUA JIPYA KUHUSU MAJENGO YA WTC BAADA YA MIAKA 13 TOKA KUSHAMBULIWA - NEW YORK

WTC
Muonekano wa majengo pacha ya One World Trade Centre, New York.

Ni wakati wa hisia tofauti kwa watu wa Marekani ambapo kwa kumbukumbu hii wapo ambao wanaumizwa kwa kupoteza ndugu, jamaa na rafiki zao waliofikia 2,700 kutokana na shambulio la kigaidi lililotokea Septemba 11, 2001 katika majengo pacha ya World Trade Centre, (WTC) New York.

Eneo lililopatwa na mkasa huo leo linatengeneza tena historia nyingine tofauti ambapo yamejengwa majengo mengine pacha yenye ghorofa 104 kila moja, huku urefu wake ni futi 1776, na thamani ya majengo hayo ni kiasi cha Dola bilioni 3.9.
WTC
Hii ni ramani ya majengo hayo yanavyoonekana kwenye mfumo wa 3D.
WTC
Muonekano wa jengo moja la One World Trade Centre katika hatua za mwisho za ujenzi.


Majengo hayo kwa sasa yanaitwa One World Trade Centre, imeripoti kuwa majengo hayo kwa sasa huenda yakawa ndiyo majengo marefu zaidi Marekani.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post