Unknown Unknown Author
Title: #FAHAMU:: WILLY SAGNOL AJITIA KITANZI KWA KUWATUSI WAAFRIKA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Meneja wa klabu ya Bordeaux ya nchini Ufaransa Willy Sagnol, amejiingiza kwenye matatizo makubwa baada ya kutoa maneno ya kashfa dhidi ya w...
Meneja wa klabu ya Bordeaux ya nchini Ufaransa Willy Sagnol, amejiingiza kwenye matatizo makubwa baada ya kutoa maneno ya kashfa dhidi ya wachezaji wanaotoka barani Afrika wakati akizungumza na vyombo vya habari mwishoni mwa juma lililopita.
Sagnol, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2006, zilizofanyika nchini Ujerumani amenukuliwa na vyombo vya habari akisema wachezaji kutoka barani Afrika wamekua na nguvu za kutosha lakini wanakosa kuwa na umakini pamoja na nidhamu.

Sagnol, mwenye umri wa miaka 37, amesema mara nyingi klabu za soka barani Ulaya zimekua na bahati ya kuwasajili wachezaji kutoka Afrika kwa kunufaika na nguvu zao lakini katika mambo mengine imekua tofauti.

"Unajua soka halimaanishi mtu kuwa na nguvu pekee yake, bali inatakiwa mchezaji awe na akili za kumkabili adui na umakini wa kucheza kwa kujituma wakati wote, kitu ambacho wachezaji wengi wa Afrika hawana."
Hata hivyo raisi wa klabu ya Bordeaux, Jean-Louis Triaud ameingilia kati suala hilo kwa kumkingia kifua meneja wake kwa kusema amenukuliwa vibaya na vyombo vya haabri na haoni sababu ya jambo hilo kukuzwa kiasi hicho.

Triaud amesema Willy Sagnol hakuwa na maana mbaya, zaidi ya kueleza anachokiona katika mchezo wa soka.

“Sasa iweje anachukuliwa kama mbaguzi?” Alihoji kiongozi huyo.

"Wachezaji wengi kutoka Afrika, huja Ufaransa wakiwa na umri mdogo na wanapata nafasi ya kukaa na wakufunzi wao, hivyo jambo kama hilo lazima lionekane, na mtu anaposema ukweli asichukuliwe kama mbaguzi.” Ameongeza Triaud

Hata hivyo Lilian Thuram ambae aliwahi kucheza sambamba na Sagnol katika kikosi cha timu ya taifa, ameonyesha kukasirishwa na kauli iliyotolewa na meneja huyo wa Bordeaux kwa kusema inawadhalilisha wachezaji wote wa Afrika.

Amesema haipendezi kwa mtu kama Sagnol, kuzungumza maneno hayo katika vyombo vya habari kwa kueleza udhaifu wa wachezaji wa Afrika na hata ni kweli, bado hakustahili kufanya hivyo kutokana na maadili ya kazi yake.

Kauli hiyo ya Sagnol, imeanza kufananishwa na ile iliyotolewa na raisi wa shirikisho la soka nchini Italia (FIGC) Carlo Tavecchio, wakati akipiga kampeni za kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo mapema mwaka huu.

Kiongozi huyo aliyeingia madarakani mwezi August mwaka huu huko nchini Italia, alifungiwa kutojihusisha na soka kwa muda wa miezi sita baada ya kukutwa na hatia ya ubaguzi wa rangi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top