Unknown Unknown Author
Title: SHIRIKA LA EGPAF LATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA TSH. MILIONI 25, HOSPITALI YA WILAYA YA KILWA - LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MKuu Wa Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi, Abdallah Ulega akiwa na Mganga mkuu wa Wilaya hiyo. Dkt Peter Nsanya wakibadilishana mawazo Mara b...
Kilwa kivinje
MKuu Wa Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi, Abdallah Ulega akiwa na Mganga mkuu wa Wilaya hiyo. Dkt Peter Nsanya wakibadilishana mawazo Mara baada ya kuwasili katika Hospital ya kinyonga kupokea msaada wa vifaa Tiba toka Egpaf
Kilwa kivinje
Baadhi ya wauguzi waliokuwa wakishuhudia kupokelewa vifaa tiba

Kilwa kivinje
Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa kwa ajili ya vipimo vya awali vya saratani ya kizazi kwa akina mama
Kilwa kivinje
Meneja Wa Egpaf Mtwara na lindi Dkt John Rithe akisoma taarifa fupi toka Egpaf katika hafla hiyo


NA. ABDULLAZIZ, KILWA
Shirika lisilo la kiserikali la EGPAF limekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 25 milioni kwa hospitali ya wilaya ya Kilwa mkoani Lindi. Halfla ya kukabidhi vifaa hivyo vitakavyotumika katika uchunguzi wa awali wa tatizo la saratani ya mlango wa kizazi kwa akinamama katika mji wa Kilwa kivinje. 

Akikabidhi vifaa hivyo ikiwamo mashine maalum ya kuchunguzia ili kutambua dalili za awali za ugonjwa huo mratibu wa afya,uzazi na jinsia wa shirika hilo, Angasyege Kibona. Alisema katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, shirika hilo lilibaini ongezeko la akinamama wenye dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi mkoani Lindi na Tanzania kwa jumla.

Kibona alisema hadi kufikia mwezi juni mwaka huu katika hospitali ya mkoa wa Lindi jumla ya wanawake 350 walipatiwa huduma ya upimaji na ugunduzi wa dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi.Ambapo wanawake 17 walikuwa wanaishi na virusi vya UKIMWI(VVU) na 14 walibainika kuwa na dalili za awali za ugonjwa huo.

Mratibu huyo aliongeza kusema kuwa katika kipindi hicho hospitali hiyo iliwapatia rufaa wanawake watatu kwenda katika hospitali ya Ocean Road kwa matibabu zaidi. Alibainisha kuwa msaada wa vifaa vya aina hiyo vinavyotolewa na shirika hilo kwa ufadhili wa shiririka lisilo la kiserikali la udhibiti wa magonjwa na kinga(CDC) lilipo chini ya msaada wa watu wa Marekani. Limetoa vifaa vya aina hiyo na kwa thamani kama hiyo kwenye hospitali wilaya ya Nachingwea na hospitali ya mkoa wa Lindi.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega licha ya kulishukuru shirika hilo kwa kutoa msaada huo muhimu kwa uhai wa binadamu. Alisema uwepo wa tatizo hilo unatishia maisha ya wanawake,hivyo baada ya kupata vifaa hivyo wanawake hawanabudi kwenda katika hospitali hiyo ili kuchunguzwa kama wanadalili za awali ambapo hakuna malipo yoyote yanayotozwa kwa ajili ya huduma hiyo.

Aidha Mkuu wa Wilaya huyo aliwataka watoahuduma katika hospitali hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na kuepuka vitendo vinavyokinzana na taaluma zao, Alisema ukiukwaji wa maadili ikiwamo rushwa,lugha chafu kwa wagonjwa vinaweza kusababisha kutofikiwa lengo na sababu ya kusaidiwa vifaa hivyo ambavyo ni msaada mkubwa wa kukabiliana na tatizo hilo.


Kilwa kivinje

Mratibu Wa afya ya uzazi na jinsia, Angesyege Kibona akikabidhi mashine ya kipimo Cha saratani ya shingo ya kizazi (CRYOTHERAPY) Kwa mkuu wa wilaya ya kilwa kwa niaba ya Egpaf
Kilwa kivinje
Dkt Juma songoro WA Egpaf (katikati) akitoa maelezo mafupi kwa mkuu wa wilaya ya kilwa kuhusiana na kipimo hicho, kulia ni Dkt John Rithe meneja Egpaf
Kilwa kivinje
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa nae akikabidhi msaada huo kwa Mganga mfawidhi kinyonga hospital Dkt Dominic kitego
Abdallah Ulega


Mkuu wa wilaya akitoa neno la shukran kwa shirika la Egpaf kwa msaada huo utakaosaidia vifo vya akina mama wilayani humo ambapo sasa Kila Vizazi 1000 vifo 190.Kulia kwake ni Mganga mkuu wa mkoa Dkt sonda yusuf na kushoto ni mkurugenzi mtendaji Kilwa, Bi Maimuna Mtanda.


Kilwa kivinje

Baadhi ya wauguzi waliokuwa wakishuhudia kupokelewa vifaa tiba


********************************************
LindiYetu.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani, Siasa, Michezo ya Africa na Nje, Tuwe pamoja huku pia >> Instagram Twitter Na Facebook

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top