Unknown Unknown Author
Title: RIO FERDINAND AIMWAGIA LAWAMA MANCHESTER UNITED...ADAI HAKUPEWA NAFASI YA KUAGA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kesho jumapili, Rio Ferdinand atarudi katika klabu yake ya zamani, Manchester United akiichezea Queens Park Rangers  RIO Ferdinand ...
Rio ferdnand

Kesho jumapili, Rio Ferdinand atarudi katika klabu yake ya zamani, Manchester United akiichezea Queens Park Rangers 

RIO Ferdinand anarudi Manchester United kwa mara ya kwanza kesho jumapili, lakini amelalamika kuwa klabu hiyo aliyoichezea kwa miaka 12 kamwe haikumpa nafasi ya kuaga kabla ya kujiunga na QPR.
Ferdinand aliichezea United mechi 455 na alitoa mchango mkubwa katika mafanikio ya Sir Alex Ferguson, lakini Mkurugenzi msaidizi Ed Woodward alimuambia baada ya mechi ya mwisho dhidi ya Southamptom msimu uliopita kuwa hataongezewa mkataba.
Baada ya kuambiwa hivyo, beki huyo mwenye miaka 35 aliondoka Old Trafford na kujiunga na QPR mwezi julai mwaka huu.
"Nilikuwa na mafanikio makubwa Old Trafford," alisema Ferdinand. "Sijawahi kupata nafasi ya kuaga nilipoondoka. kilikuwa kitendo kibaya, kwahiyo nitapata fursa ya kuwaaga watu wengi walionisapoti na kunisaida" 

Rio ferdnand
Beki huyu alijiunga na Harry Redknapp katika dimba la Loftus Road majira ya kiangazi baada ya kutumika kwa miaka 12 Old Trafford 
Rio ferdnand
Ferdinand aliiwakilisha vyema Manchester United kwa muongo mmoja na alibeba makombe sita ya ligi kuu

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top