NDOA YA AMBER ROSE NA WIZ KHALIFA YAFIKIA KIKOMO, BAADA YA KUISHI KWA MWAKA MMOJA

Wiz khalifa na Amber Rose
Tmz wameripoti kuwa model Amber Rose ameomba talaka kutoka kwa mume wake ambaye wameishi pamoja kwa muda wa mwaka moja. Amber anasema yeye na mumewe wametengana kuanzia Jumatatu na anataka haki zote za malezi za mtoto wao Sebastian mwenye umri wa mwaka mmoja.

Tofauti na ndoa za wasanii wengine zikivunjika hugawana pesa na mali, Amber alisainishwa makubaliano ya kutochukua mgao wa pesa au mali kutoka kwa mumewake endapo watatengana.

********************************************
LindiYetu.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani, Siasa, Michezo ya Africa na Nje, Tuwe pamoja huku pia >> Instagram Twitter Na Facebook

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post