Wateja wa NSSF wakipata huduma na Maelezo ya Shirika hilo Ndani ya Viwanja vya maonesho ya Nane Nane - Ngongo Mkoani Lindi, Ambapo maonesho hayo yanafanyika Kitaifa kwa mwaka Huu.
Wateja wa NSSF wakipata huduma na Maelezo ya Shirika hilo Ndani ya Viwanja vya maonesho ya Nane Nane - Ngongo Mkoani Lindi, Ambapo maonesho hayo yanafanyika Kitaifa kwa mwaka Huu.
Wananchi wameombwa kujiunga na mfuko wa taifa wa jamii, NSSF ili waweze kupata mikopo yenye masharti na riba nafuu itayowazesha kujikwamua katika lindi la umaskini.
Wito huo umetolewa na ofisa mwandamizi sekta isiyorasmi wa mfuko huo,Salim Kimaro alikuwa anaeleza faida za mfuko huo hapo jana kwa waandishi wa habari katika maonesho ya nanenane yanayoendelea katikaviwanja vya Ngongo manispaa ya Lindi.
Kimaro alisema mfuko huo kwakutambua umuhimu wa wananchi wenye kipato cha chini katika kuchangia maendeleo ya taifa na maendeleo yao binafsi ya kiuchumi kupitia kazi wanazozifanya ikiwamo kilimo na ufugaji.
Mfuko huo unawezesha kupata kupata mikopo kwa masharti na riba nafuu wanayomudu kuirejesha wakiwa wamepata faida. Alisema licha ya kuwapatia mikopo yenye masharti na riba nafuu, lakini pia mfuko huo unamasharti rahisi ya kujiunga lengo likiwa ni kuwafanya wananchi wengi waweze kujiunga na kufaidi fursa zinazotokana na mfuko huo.
Alisema kutokana na mfuko huo kuwa rafiki na mkombozi kwa wananachi,idadi ya watu wanaojiunga inaongezeka kwa kasi. Kitendo ambacho kinaongeza ari ya kuwahudumia kwa ufanisi iliwasijute kwa uamuzi wao wa kujiunga kwenye mfuko huo.
Ofisa mwandamizi huyo alisema: kikwazo kikubwa kinachosababisha wananchi wengi ikiwamo wakulima kushindwa kupata mikopo ni masharti magumu na riba kubwa kutoka kwenye taasisi za fedha ikiwa mabenki.
"wakulima wanaweza kupata mikopo kupitia saccos,na hata kuhusu huduma za matibabu sifa ya matibabu ukomo ni mpaka kuzeeka mfuko huu nikwaajili ya waTanzania wote bila kumbagua yeyote."alisema Kimaro.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.