Unknown Unknown Author
Title: ICC KUJENGA UKUMBI WA KISASA LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
NA-ABDULAZIZ.LINDI Wananchi wameombwa kutumia kituo cha kimataifa mikutano cha Arusha (ICC) na vituo vingine vinavyo milikiwa na shirika...
NA-ABDULAZIZ.LINDI
Wananchi wameombwa kutumia kituo cha kimataifa mikutano cha Arusha (ICC) na vituo vingine vinavyo milikiwa na shirika hilo ni kwa ajili ya mikutano ya kimataifa pekee, na kuachana na dhana ya kuwawatumiaji kumbi hizo mashirika na taasisi kubwa hasa za kimataifa.

Wito huo umetolewa na ofisa mkuu wa masoko na utafiti wa shirika la AICC, Linda Nyanda alipozungumza na waandishi wa habari waliotembelea banda la shirika hilo kwenye maonesho ya nanenane yanayofanyika manispaa ya Lindi kitaifa.

Nyanda alisema Shirika la ukumbi wa mikutano wa kimataifa AICC limepanga kujenga ukumbi wa kisasa katika mikoa ya Lindi/Mtwara wenye hadhi na viwango vya kimataifa ili kukidhi mahitaji kwa ya watumiaji wa nje na ndani, na kwa lengo la kuondokana nadhana ambayo haina ukweli kwani vituo hivyo vipo kwa ajili ya kuwa hudumia watumiaji wa ndani na nje wenye kipato kikubwa pekeee.

Alisema kwa kuzingatia ukweli kwamba shirika hilo linatoa huduma kwa watumiaji wenye vipato tofauti, linazo kumbi zenye uwezo wa kutumiwa na idadi ya watu 10300.
"wananchi wasiogope kuja na kutumia kumbi zetu kwa ajili ya mikutano kwani zipo kumbi ambazo zinaendana na mahitaji na kipato cha mtumiaji,kwazingatia hilo shirika lina kumbi ndogondogo kumi zenye uwezo wa kutunza kumi hadi miatatu"alisema Nyanda.
Alisema kwa kuwa kilimo ni biashara nijambo lisilo na shaka kuwa wakulima pia ni wadau wa vituo hivyo vya mikutano ikizingatiwa kwamba wanunuzi wa mazao wanayozalisha ni wa ndani na nje. Hivyo mipango mbalimbali inayohusiana na sekta hiyo inaweza kufanyika kwenye vituo hivyo vya mikutano.
"watembelee vituo vyetu ndipo watathibitisha ukweli wa hayo kwani hata bei kwa watumiaji wa ndani na nje zinatofautiana sana,bei kwa mikutano ya ndani ni nafuu kuliko mikutano ya kimataifa"alifafanua Nyanda.
Ofisa mkuu huyo wa masoko na utafiti alibainisha kuwa katika kujipanua kibiashara na kufikisha huduma kwa wananchi wengi shirika hilo limejenga nyumba nyumba 17 zilizopo eneo la Faya jijini Arusha ambazo zimepangishwa, na nyumba tatu zilizopo eneo la Korido ambazo pia zimekodishwa.

Nyanda alisema katika kuhakikisha shirika linakuwa na vituo vya kisasa vitakavyo himili ushindani katika soko la ndani na nje linampango wa kujenga kituo kingine cha mikutano cha kisasa ambacho kitakuwa na huduma zote zenye ubora na hadhi ya kimataifa ambapo hatua za awali za ujenzi wake zimeanza katika jiji la Arusha.

Aidha alisema kwa kuwa kilimo ni biashara nijambo lisilo na shaka kuwa wakulima pia ni wadau wa vituo hivyo vya mikutano ikizingatiwa kwamba wanunuzi wa mazao wanayozalisha ni wa ndani na nje, hivyo mipango mbalimbali inayohusiana na sekta hiyo inaweza kufanyika kwenye vituo hivyo vya mikutano.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top