Unknown Unknown Author
Title: TISHIO LA UGONJWA WA EBOLA, WANANCHI WATAKIWA KUJIHADHALI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Pichani ni baadhi ya Daktari wakiwa wamembeba mgonjwa wa EBORA picha kwa hisani ya Mtandao. Na Hannah Mayige, wa Chuo Kikuu Huria, OU...
Pichani ni baadhi ya Daktari wakiwa wamembeba mgonjwa wa EBORA picha kwa hisani ya Mtandao.

Na Hannah Mayige, wa Chuo Kikuu Huria, OUT
TISHIO la ugonjwa wa Ebola unaoendelea kuuwa mamia ya watu Afrika Magharibi, umezua wasiwasi mkubwa kwa nchi za Afrika na dunia nzima kwa ujumla na kutakiwa watanzania kuchukua tahadhari kubwa kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini.

Lazima Serikali na wananchi wazingatie masharti na tahadhari inayotolewa kimataifa kuudhibiti ugonjwa na utayari wake wa kupambana nao.

Ugonjwa wa Ebola, umekuwa tishio kubwa kwa uhai na ustawi wa mataifa mbalimbali yakiwemo ya Afrika Mashariki ambako Tanzania ni mojawapo.
Mpaka sasa, nchi zilizoathirika na ugonjwa huo ni pamoja na Cameroon, Liberia na Nigeria ambapo tayari zaidi ya watu 1,000 wamepoteza maisha.

Eneo la Afrika mashariki, kuna taarifa kuwa hivi karibuni alipatikana mgonjwa wa Ebola katika nchi ya Rwanda na kwamba miaka ya nyuma milipuko iliwahi kutokea nchini Uganda.

Ebola ni ugonjwa ambao mpaka sasa hauna tiba wala chanjo, ambapo huambukiza kwa njia ya hewa au majimaji yatokayo mwilini kama mate, jasho, damu na kwamba mgonjwa akigusana na mtu asiye na virusi hivyo basi anaambukizwa.

Shirika la Afya Duniani [WHO] limetahadharisha nchi mbalimbali hasa Afrika kuchukua tahadhari kubwa, mfano hivi karibuni ndege za shirika la Kenya lilishauriwa kutoendelea na safari zake za Afrika Magharibi kwa kuhofia baadhi yaabiria wake kuhamisha virusi vya Ebola na kusambaza katika eneo la Afrika Mashariki.
Kenya ni mojawapo ya nchi za Afrika mashariki zenye safari nyingi za ndege kuelekea mataifa mbalimbali.

Kutokana na wito huo wa WHO, tayari Korea imesitisha safari zake za ndege kwenda Kenya kwa tahadhari ya kudhibiti usambaaji wa Ebola.
Kwa kuwa ugonjwa huo unaambukiza kwa njia ya hewa pia na majimaji yatokayo mwilini hata madaktari na wauguzi wanalazimika kuwa na mavazi maalum ambayo yanafunika mwili mzima, kwani hawatakiwi kugusana kwa namna yeyote ile.

Msimamizi wa Vituo vya Afya mipakani Tanzania, Dk. Khalid Massa, anasema vifaa hivyo ni pamoja na magauni, aproni, buti, gloves na vifaa maalum vya kuziba pua na mdomo.

“Wahudumu wanatakiwa kuvaa vifaa hivyo kujikinga na maambukizi na tayari vifaa 20,000 vimepokelewa na kusambazwa katika maeneo yaliyoainishwa,” anasema Dk. Massa.
Dk. Massa, anasema kwa kushirikiana na maofisa uhamiaji wamejikita zaidi kuchunguza wasafiri wa ndege hasa wanaotokea Afrika Magharibi.
Naye, Mtaalamu wa Kudhibiti magonjwa ya mlipuko Dk. Vida Makundi, anawaasa wananchi kuripoti mapema katika vituo vya afya au kwa viongozi wa serikali za mitaaa endapo watakuwa na dalili za ugonjwa huo.

Anazitaja dalili kubwa ambazo zimeelezwa na Shirika la Afya duniani ni pamoja na kuumwa sana kichwa , kupata homa kali, na hatimaye kutokwa na damu katika maeneo yenye uwazi, kama vile mdomoni, ngozi, masikioni na sehemu za siri.

Ebola imesababisha hofu na tafrani kubwa kwa nchi hasa zinazoendelea kwa kuua watu bila kupata tiba ikiwa ni pamoja na madaktari na udhoofisha hali ya uchumi kutokana na shughuli nyingi za kusafiri na zinazokutanisha watu kusitishwa.

Shughuli za biashara za kimataifa pia zinaendelea kutetereka kuogopa maambukizi ya virusi vya Ebola hasa wananchi katika nchi zenye ugonjwa huo kuogopana wenyewe kwa wenyewe.

Mfano, huko Cameroun, kuna mtu alikutwa amekufa barabarani hakuna mtu aliyethubutu kumsogelea mpaka walipokuja madaktari ambao walivalia rasmi kuhakikisha hakuna maambukizi mapya kwa watu wengine.

Hapa Tanzania, tayari serikali kupitia viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais Mohamed Ali Bilal , Waziri wa Afya Dk. Seif Rashid na baadhi ya wakuu wa mikoa ya Manyara, Dar es Salaam na Mbeya wamewataka wananchi kuwa waangalifu na wageni wasio wajua na kuwa tahadharisha kwenda hospitali mara wanapoona wana dalili zisizo za kawaida au zinazoashiria ugonjwa wa Ebola.

Kulingana na tamko la serikali, Ebola bado haijaingia nchini lakini usemi wa Kiswahili usemao ‘ukiona mwenzako ananyolewa, wewe tia maji’.


Kwa upande wa kutenga maeneo maalum ya kushughulikia wagonjwa wa Ebola, serikali imetenga maeneo mawili kwa Dare s Salaam, Temeke na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Waziri wa afya DK. Seif Rashid anasema tayari wauguzi na madaktari wanapatiwa elimu kuhusiana na kuudhibiti ugonjwa wa Ebola kabla haujaingia nchini, elimu hiyo inatolewa katika hospitali zote .

Nao, wananchi kwa nyakati tofauti wameendelea kumlilia mungu kwa mlipuko wa magonjwa hapa barani Afrika. “Mara ukimwi, mara Dengue mara Ebola yote hakuna tiba,” analalamika mmoja wa wananchi Kasian Komba mkazi wa Songea.

Kutokana na taarifa za baadhi ya wananchi wa Liberia kuvamia kituo kilichotengwa kuhudumia wagonjwa wa Ebola na kupora magodoro, vifaa na wagonjwa kutawanyika, ni taarifa mbaya na huenda imetokana na kukosa elimu ya ugonjwa huo.

Kwakuwa elimu ni muhimu, ni vyema serikali hapa nchini ikatumia fursa hii kuelimisha umma kwa kutumia mikutano ya hadhara, Sanaa za maonesho, mabango, vyombo vya habari kama mitandao ya kijamii, redio, televisheni, magazeti na vipeperushi ili jamii ipate uelewa.

Makala hii imeandikwa na Hannah Mayige, Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania – OUT.
Anapatikana kwa E-mail hannahmayige@gmail.com

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top