FIESTA 2014 na KTMA TOUR, MBONA KAMA MNASHINDANA....!!! KUNANI?

Mpenzi Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
WASANII
Fiesta imeandaliwa chini ya uzamini wa bia ya Serengeti (SBL) na Kili Music Tour imedhaminiwa na bia ya Kilimanjaro (TBL). 

Wote wanafanya kazi nzuri kwa wasanii wetu, na inawapa ajira na kipato wabongo!!

Swali langu, kwanini msingepeana nafasi mmoja aanze na mwingine amalizie kuliko mnachofanya sasahivi, huku kuna Fiesta kule kuna Kili Tour??? 
Ila binafsi ninaona kama mnashindana ambako hakuna sababu yeyote ile..ni kwa faida ya nani??? 
Wote mnataka kuwatumia wasanii wale wale na sehemu zile zile.

Nadhani mngewanufaisha wasanii wetu na kutoa fursa kwa watu wengi kama mngepeana nafasi mmoja aanze na mwingine amalizie....kuliko hivi mnavyofanya.

Mfano Fiesta ilianzia Mwanza...Kili Tour ikawa Mbeya the same weekend!!! WHY???

Kila brand ingetafuta muda sahihi na sio kukomoana, mnawanyima fursa wasanii na wapenzi wa burudani.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post