
Mgahawa uliolipuliwa na Bomu Jijini Arusha

Baadhi ya watu waliojeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu uliotokea jana usiku katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Selian, jijini Arusha kwa matibabu.

WATU nane, wengi wao wakiwa ni wa asili ya Asia, wanahofiwa kujeruhiwa vibaya kwa bomu lililotupwa kwenye mgahawa uliopo eneo la Gymkhana jijini Arusha usiku wa kuamkia leo.

Jeshi la Wananchi likishirikiana na Jeshi la Polisi wanachunguza chanzo cha bomu hilo.
Tags
HABARI ZA KITAIFA