Nyota mpya wa Arsenal, Alexis Sanchez akiwa ndani ya 'uzi' mpya.
MSHAMBULIAJI mahiri wa Chile na Barcelona, Alexis Sanchez, amejiunga na Klabu ya Arsenal kwa pauni milioni 30 na mkataba wa miaka miaka minne.
Alexis Sanchez atakuwa Arsenal kwa miaka minne.
Akiwa klabuni hapo, nyota huyo atalipwa pauni 140,000 kwa wiki sawa na Mesut Ozil aliyekuwa analipwa kiasi hicho kikubwa kuliko wote ndani ya timu hiyo ya London.
Sanchez atalipwa pauni 140,000 kwa wiki sawa na Ozil.
Sanchez amekatiza likizo yake kukamilisha uhamisho huo na kufanyiwa vipimo ambapo mkataba wake huo una kipengele cha uwezekano wa kuongeza miezi 12 zaidi.
Kwa kujiunga na mabingwa hao wa Kombe la FA, Sanchez amemwandalia mazingira mazuri mshambuliaji wa Liverpool na Uruguay, Luis Suarez kutua Barcelona kuziba pengo lake kwa uhamisho wa pauni milioni 75.
Arsenal wabovu tu hata wamsajili nani
ReplyDelete