Unknown Unknown Author
Title: MWILI WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KINYAMA KWA WIVU WA KIMAPENZI WAOKOTWA MKOANI LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga. MWILI wa mwanamke mwingine aliyetambulika kwa jina la Zuhura Mtenda mwenye umri wa mi...
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga.

MWILI wa mwanamke mwingine aliyetambulika kwa jina la Zuhura Mtenda mwenye umri wa miaka, 32 umeokotwa jana na kufanya idadi ya wanawake waliouawa mpaka sasa katika Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kufikia nane.

Wanawake hao nane waliouawa kikatili mpaka sasa wana umri kati ya miaka 18-32.
Chanzo cha mauaji hayo kimedaiwa kuwa ni uhusiano wa kimapenzi.

Katika kuonyesha kuwa wamekerwa na vitendo hivyo, baadhi ya wananchi wilayani humo, walizingira Kituo Kikuu cha Polisi Nachingwea, kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nne wakitaka polisi kuwaruhusu kuwa waue watuhumiwa watatu wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo ambapo polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga, amesema wananchi hao wenye hasira walikuwa wamezunguka kituo hicho cha polisi wakitaka kuwaua watuhumiwa watatu wanaoshukiwa kuwa ndio wahusika wa baadhi ya mauaji ya wanawake hao.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top