Mkuu wa wilaya ya Lindi Dkt Nassoro Ally Hamidi akimpokea Mkimbiza mwenge wa Uhuru Ndg Rechel Stephen Kasanda
Na. Mwandishi Wetu
Hapo jana Mnamo saa 8:15 asubuhi Manispaa ya Lindi iliweza kuupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi katika Viwanja vya Shule ya msingi Mnazi mmoja na Kuweza kuukimbiza sehemu kadhaa katika eneo la Manispaa hiyo kwa ajili ya Kuweka Mawe ya msingi na Kufungua Miradi mbalimbali ya Jamii na Ile iliyosimamiwa na Serikali. Mbio hizo za Mwenge kwa Mwaka wa 2014 zilikuwa zikiongozwa na Ndg Rechel Stephen Kasanda pamoja na Viongozi wa Mkoa alikuwepo Mkuu wa Wilaya ya Lindi Dkt. Nassoro A. Hamidi, Mkurungezi wa Manispaa ya Lindi Ndg Kelvin Makonda na Viongozi wengine.
Katika Kukagua Miradi mbali mbali katika Kata mbalimbali za Manispaa ya Lindi Kiongozi huyo wa Mbio za mwenge aliweza kuwapongeza wakazi wa Kijiji cha Nandambi kwa kuweza kujitolea kwa hali na mali na Kufanikisha Ujenzi wa Zahatani ambayo aliweza kuiwekea jiwe la msingi ikiwa kiasi kikubwa cha pesa cha Ujenzi huo kinatoka kwa Wananchi wenyewe na aliwataka wasife moyo waendelee na moyo huo hadi kufanikisha Ujenzi huo unakamilika, Pia aliweza kumpangeza Mh. Diwani wa Kata hiyo kwa kuweza kuwashawishi wananchi hao kushiriki katika shughuli za kujitolea ili kujiletea Maendeleo katika kata yao.
Pia Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge aliwasihi kushiriki katika Mchakato wa Utoaji maoni ya Katiba ya Nchi pindi itakapoletwa kwao kwani ndio msingi na Mhimili wa nchi yetu na aliwasihi kutorubuniwa na wanasiasa wachache wasio itakia mema nchi yetu kwa kushiriki katika hali yoyote ya kuondoa amani ya nchi hii.
Mbio hizo za Mwenge zimemalizika leo kwa Mwenge huo wa Uhuru kuukabidhi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara.
Hizi ni Picha Mbalimbali za Miradi iliyowekwa mawe ya Msingi na Ufunguzi.
1. MARADI WA MAJI MINGOYO -UJENZI WA TANKI LA KUHIFADHIA MAJI
Wafanyakazi wa Kata ya mingoyo na wajumbe wa Mradi wa Ujenzi wa Tangi la Maji Kata ya mingoyo wakiwa katika bashasha kubwa tayari kwa ajili ya uwekwaji wa Jiwela Msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg. Rechel Stephen Kasanda.
Mjumbe akisoma Taarifa ya mradi wa Ujenzi wa Tangi la maji katika Kata ya Mingoyo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndg. Rechel Stephen Kasanda
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg. Rechel Stephen Kasanda akikata utepe kuashirria kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa Ujenzi wa tangi la maji kwa wakazi wa Kata ya Mingoyo.
2. MRADI WA UJENZI WA MAABARA SEKONDARI NG'APA
Jengo la Maabara la Shule ya Sekondari ya Ng'apa likiwa Tayari kabisa Kufunguliwa na Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Ndg. Rechel Stephen Kasanda
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndg. Rechel Stephen Kasanda akisisitiza jambo mara baada ya ukaguzi wa jengo la maabara ya Shule ya Sekondari Ng'apa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndg. Rechel Stephen Kasanda akikata Utepe kuashiria Kulifungua Jengo la Maabara ya Shule ya Sekondari Ng'apa
3. MRADI WA UHIFADHI WA MSITU - NANDAMBI MKANGA 1
Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Ndg Kelvin Makonda (aliyevaa kofia nyeupe) akiwa sambamba na Afisa utumishi wa Manispaa hiyo ya Lindi wa kisoma Ramani ya Msitu wa Hifadhi Nandambi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg. Rechel Stephen Kasanda akipata maelekezo kutoka kwa afisa wa misitu katika usomaji wa ramani ya eneo la hifadhi ya Msitu.
4. MRADI WA UJENZI WA KARAKANA YA USELEMALA - KILOLO NANDAMBI
Wanakikundi wa MkambaKamba Fenicha wakiwa tayari kuifungua Karakana yao ya Ufundi Seremala katika kijiji cha Kilolo Nandambi
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg. Rechel Stephen Kasanda akikata Utepe kuashiria kuifungua karakana ya Kikindi cha mafundi Seremala wa Kilolo kijiji cha Nandambi.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg. Rechel Stephen Kasanda akijaribu kuranda mbao kwa Kutumia kifaa cha Kisasa kabisa kinachopatikana kwenye Karakana ya Kilolo kijiji cha Nandambi wakati wa Ufunguzi wa Karakana hiyo.
5. MRADI WA UJENZI WA ZAHANATI - NANDAMBI
Wananchi wa Kijiji cha nandambi wakiwa wamejipanga tayari kuushika Mwenge wa Uhuru katika Sherehe ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Zahanati ya Kijiji hicho.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndg. Rechel Stephen Kasanda akisikiliza Taarifa ya ujenzi wa Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Nandambi ambalo aliliwekea jiwe la msingi
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru akichanganya Zege wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi Katika Zahanati ya Kijiji cha Nandambi Manispaa ya Lindi
6. MRADI WA UJENZI WA OFISI YA KIJIJI MKANGA
Wananchi wa Mkanga wakiwa wamekusanyika kwa wingi kushuhudia Ufunguzi wa jengo la Ofisi ya Kijiji Hicho.
Wananchi wakiwa wenye Furaha katika ufunguzi wa jengo la Ofisi ya Kijiji cha Mkanga, Jengolililofunguliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg. Rechel Stephen Kasanda Akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo la Ofisi ya kijiji cha Mkanga ndani ya Manispaa ya Lindi
7. MRADI WA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA- S/M KINENG'ENE
Wanafunzi wa Shule ya msingi ya Kineng'ene waliweza kuushika mwenge wa Uhuru wakati wa Ufunguzi wa Madarasa mawili ya Shule hiyo
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndg. Rechel Stephen Kasanda akikagua Madarasa ya Shule ya msingi ya Kineng'ene wakati wa Ufunguzi
Ndg. Rechel Stephen Kasanda Akikata Utepe katika Moja ya madarasa yaliyojengwa
8. MRADI WA NYUMBA YA DAKTARI - KATA YA NACHINGWEA
Nyumba ya Daktari wa Zahanati ya Kata ya Nachingwea nayo ilifunguliwa na Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg. Rechel Stephen Kasanda akikata utepe kuashiria amefungua Nyumba hiyo ya Daktari wa zahanati ya Kata ya Nachingwea Mjini Lindi
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.