Unknown Unknown Author
Title: BREAKING NEWS:: BUSI LA 5 ALLIANCE LANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO - MNAZI MMOJA, LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Bus linalofanya safari za kusafirisha abiria kutoka Dar kuelekea Mtwara lenye Namba za Usajili T 667 CLY Mali ya Kampuni ya 5 Alliance l...
ajali ya moto katika bus
Bus linalofanya safari za kusafirisha abiria kutoka Dar kuelekea Mtwara lenye Namba za Usajili T 667 CLY Mali ya Kampuni ya 5 Alliance limenusurika kuteketea na Moto hivi Punde katika Eneo la Mizani iliyopo Kijiji cha Mnazi Mmoja kata ya Mingoyo Mkoani Lindi.
ajali ya moto katika bus
Shuhuda wa Tukio hilo anaeleza kuwa Gari hilo lilifika Kituoni hapo likiwa na abiria na likiwa katika harakati za kupimwa uzito ndio Watu wa Nje walishuhudia Moto Ukiwaka kutokea Chini ya Gari hilo na Kuwapigia kelele wenye Bus na kufanikiwa Kuudhibiti moto huo kabla ya Madhara makubwa kutokea. 
ajali ya moto katika bus
Halihiyo iliwafanya abiria wa Busi hilo kushikwa na Taharuki na kutoka ndani ya Bus hilo kwa Haraka sana kwa kuhofia kupoteza maisha yao na maliwalizonazo, Taarifa inaelezwa kuwa hakuna Majeruhi waliotokana na ajali hiyo na Hata hivyo tatizo lililekebishwa na Bus hilo liliweza Kuruhusiwa kuendelea na Safari hiyo ya kuelekea Manispaa ya Mtwara Mikindani.
ajali ya moto katika bus
Baadhi ya Abiria walioshuka katika Basi Hilo wakishuhudia jitihada za kuudhibiti moto huo uliotaka kuteketeza basi hilo

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top