POLISI WAPAMBANA NA WAANDAMANAJI BRAZIL

lindiyetu news
Polisi katika mjini wa São Paulo nchini Brazil wametumia mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji wanaopinga Kombe la Dunia, ikiwa ni saa chache tu kabla ya michuano hiyo kuanza.

Taarifa zinasema mtu mmoja amekamatwa na mwandishi mmoja wa CNN kujeruhiwa.Waandamanaji wanasema wamepanga kuandamana karibu na uwanja ambao shughuli ya ufunguzi itafanyika.

Maandamano zaidi yamepangwa katika miji mingine ya Brazil kupinga michuano hiyo kuandaliwa nchini humo.

Picha za TV kutoka São Paulo zinaonesha polisi wa kutuliza ghasia wakitumia mabomu ya machozi na risasi za mpira karibu na uwanja wa Corinthians.

Waandamanaji hao wamekuwa wakiimba- wakisema "hakutakuwa na kombe hapa".

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post