MWANZA HALI SI SHWARI MABOMU YA MACHOZI YARINDIMA.

JESHI la Polisi mkoani Mwanza, limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga waliokuwa wakipinga kuondolewa katika eneo la Kempu na eneo la soko la Makoroboi jijini Mwanza. ...

Hatua hiyo imesababisha vurugu kubwa na kusimamishwa kwa shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwemo kufungwa kwa maduka hadi katikati ya eneo la jiji na baadhi ya huduma ya usafiri kukosekana kwa muda katika barabara zinazokatiza katikati ya jiji kuanzia saa nne asubuhi ....

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Valentino Mlowola, amedai kuwa Jeshi hilo limelazimika kutumia mabomu hayo ili kuwatawanya wafanyabiashara hao waliokuwa wakihatarisha amani na kwamba hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kujeruhiwa katika vurugu hizo.

Baadhi ya barabara za mwanza zikiwa nyeupe yaani no gari wala bodaboda baada ya askari kutimuana na wamachinga.

1 Comments

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

  1. Tanzania tunaenda wapi jaman Tii sheria bila shuruti

    ReplyDelete
Previous Post Next Post