Unknown Unknown Author
Title: MMILIKI TAJILI WA CLUB MOJA YA KIINGEREZA ASIEKUWA NA JINA. JE WATAKA KUMJUA? BOFYA HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Katharina Liebherr: Na. Paul Manjale Jina hili la mama huyu kibonge si maarafu sana katika vichwa na midomo ya wapenda soka duniani ...
katharina loebherr
Katharina Liebherr:

Na. Paul ManjaleJina hili la mama huyu kibonge si maarafu sana katika vichwa na midomo ya wapenda soka duniani hasa bongo,labda ni kwa sababu ya jinsia yake ama ni kutokana na tabia yake ya kujiweka mbali na vyombo vya habari??

Katharina ni binti wa marehemu billionea Marcus Liebherr aliyefariki mwaka 2010 kwa ugonjwa wa moyo (heart attack) ambapo mwaka mmoja nyuma yaani 2009 billionea huyu alitoa £14m tuu kuinunua klabu machachari ya Southampton iliyokuwa karibu kufilisika.

Klabu ya Southampton ndiyo klabu ambayo ina mchango mkubwa katika uanzishwaji wa vilabu viwili maarufu vya Hispania.Klabu hii ndiyo iliyokuwa ikiviuzia jezi vilabu vya Atletico Bilbao na majirani zao Atletico Madrid miaka ile ya 1889-1950.

Klabu hii ndiyo iliyomkuza na kumuibua nyota ghali zaidi duniani kwa sasa Gareth Bale,pamoja na mapacha wawili Theo Walcott na Alex Oxlade Chamberlain.

Je,Katharina ni nani hasa mpaka nimzungumzie??Huyu ndiye bosi wa akina Victor Wanyama,Adam Lallana,Luke Shaw na Morgan Schneiderlain kwa lugha nyepesi na rahisi zaidi huyu ndiye mmiliki wa klabu ya Southampton.

Huwezi kumpata Shaw ama Lallana bila ya mama huyu kuridhia,mama huyu anamwita mmiliki wa Chelsea jina lake la kwanza yaani Roman na jamaa hachukii.Kiti anachokalia mama huyu, Wenger na Mourinho hawakalii....pesa IPO!!Vijana wake kibao wako Brazil kwenye mshikemshike wa kombe la dunia .....Upo?

Basi katika orodha yako ya wamiliki wa vilabu England ongeza na jina la huyu mwanamama wa kiswiss

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top