Unknown Unknown Author
Title: BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AIWEKA PAZURI TANZANIA KIMATAIFA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto 'kushoto' akiongoza mashabiki na wapenzi wa mchezo wa masumbwi kumpokea Ibrahimu Class...
bondia king class mawe
Mkuu wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto 'kushoto' akiongoza mashabiki na wapenzi wa mchezo wa masumbwi kumpokea Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  aliyeshika mkanda baada ya kurudi na mkanda wa WPBF kwa kumpiga Mzambia Mwansa Kabinga katika uwanja wa Arthur Davis mjini Kitwe, Zambia, kwa KO  ya raundi ya 9 na kufanikiwa kunyakuwa ubingwa huo. Wa pili  kushoto ni bondia Shomari Milundi, kulia ni Promota aliyefanikisha safari hiyo Yaj Msangi, wadau Bilali Ngonyani na Rogers Masamu 
-----------------------------
Bondia Mtanzania anaeshika rekodi  namba moja nchini Ibrahimu Class 'King Class Mawe' amerudi na ubingwa wa WPBF  nchini akitokeza Zambia ambapo alifanikiwa kumpiga kwa K,O mbaya sana bondia Mwansa Kabinga wa Zambia mchezo uliochezwa Arthur Davis Stadium, Kitwe, Zambia
Akizungumzia safari yake ya kuelekea kunyakuwa ubingwa huo alisema amepata tabu sana wakiwa njiani ambapo wame ondoka alhamisi usiku sana na kufika Jumamosi asubuhi nchini Kenya ambapo alizuiwa kutokana na kuwa na passport ndogo hivyo hakufanikiwa kwenda Zambia. Hapo Nairobi wakasaidiwa na  Balozi wa Tanzania nchini Kenya, hat hivyo ndege waliyokuwa wapande ilikuwa imeshaondoka zamani

Baada ya hapo kuna pesa  walitakiwa waongeze,  wakaongeza kiasi kwa kudunduliza ndipo wakasafiri mpaka Zambia.
bondia king class mawe
Huo ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza kucheza nje ya nchi tangia ajiunge na ngumi za kulipwa na kufanikiwa kunyakuwa ubingwa huo ambao umemuweka katika ramani nyingine kabisa ya kimataifa. 
Bondia huyo  alishukuru kwa kupokelewa na Mkuu wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto aliyekuja kwa niaba ya Serikali na kuahidi kumpatia mmoja ya michezo Kibondo au nchi jirani kwa ajili ya kumtangaza zaidi na kuendeleza kipaji chake hicho
Mkuu huyo wa Wilaya alisema "Watu wengi wanapenda mchezo wa ngumi hivyo kwa niaba ya serikali nitafanya jitiada nikupatie mchezo mmoja kwa ajili ya kutetea mkanda wako hata burundi ili uzidi kufahamika na kukuza kipaji chako"

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' hajawa nyuma kuwashukuru makocha wake ambao wamemwezesha kufika hapo ambao ni pamoja na Habibu Kinyogoli 'Masta',  Kondo Nassoro, Sako  Mtulya na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anamtafutia mapambano mbalimbali na humpa ushauri.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top