
Kijana mmoja ambaye hakuweza kujulikana mara moja jina wala wapi anapoishi amekutwa amefariki katika Kata ya Mingoyo Manispaa ya Lindi katika eneo la Liteta.

Kijana huyo aliweza kuokotwa alfajri ya leo katikati mwa barabara kuu na baada ya kumchunguza ilibainika ameshafariki na Mwili wake ukiwa unamajeraha hasa Sehemu ya Kichwani na kuonesha kuwa Kijana huyo aligongwa na Gari Majira ya Alfajiri.

Kamanda wa Polisi wa Kituo cha polisi cha Mingoyo Juma Solomon ameweza kuthibitisha tukio hilo na kusema hadi sasa halijajulikana ni gari gani lililoMgonga mtu huyo. Hivyo uchunguzi Bado unaendelea.

Naye Mtendaji wa Kata hiyo ya Mingoyo Bi. Maimuna H. Kawimba aliweza Kutoa taarifa kwa wakazi wa Kata hiyo kupitia kwa watendaji wa Vijiji waweze kuwataarifu wananchi/wakazi wa Kata hiyo Kuja kuutambua Mwili wa marehemu Kabla ya Kupelekwa Hospitali ya Mkoa Sokoine Baada ya Kukosa Ndugu aliyeweza kumtambua.



Hadi sasa Mwili wa Marehemu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Lindi ya Sokoine hadi hapo ndugu watakapojitokeza kuutambua mwili wa marehemu.

Tags
HABARI ZA KITAIFA
Rest in peace
ReplyDelete