Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa Habari Lindi akipimwa afya yake na
daktari wa NHIF Timoth Mwasajone katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa
Habari.
PICHA Ya Pamoja kati ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Mfuko wa NHIF
Mara baada ya mfuko huo kujitolea kupima Afya za waandishi wa Lindi
Mwandishi wa Tbc Lindi Martina Ngulumbi akimpokea mtoto mama alietoka
kujifungua siku ya uhuru wa habari
Mwenyekiti wa LPC ,Abdulaziz Ahmeid akikabidhi msaada Kwa Muuguzi wa zamu Bi
Habiba Chitanda msaada uliotolewa na Wanahabari wa Lindi
Mwenyekiti akisalimia baadhi ya watoto wanaogua katika wodi ya watoto Sokoine
Hosp mara baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali katika kusaidia jamii siku ya
uhuru wa habari
WANAHABARI mkoa wa Wa Lindi wakiongozwa na Mwenyekiti wao wameadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kwa kutoa msaada kwa jamiii baada ya kutoa msaada wa Vifaa mbalimbali katika wodi za wazazi na watoto katika Hospital ya Rufaa ya Sokoine Mkoani Lindi
Sambamba na wanahabari hao kushiriki katika kutoa msaada huo pia wanahabari hao waliwezeshwa kupimwa Afya zao na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani humo ili kila mmoja afanye kazi zake huku akijua Afya yake
Akiongea baada ya hafla hizo,Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Humo,Abdulaziz Ahmeid alieleza kuwa katika maadhimisho hayo ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Arusha ambayo yana kauli mbiu ya Uhuru wa Habari kwa maendeleo na utawala bora Ambapo wanahabari wameamua kurudi kwa jamiii kwa kuona umuhimu wa kusaidia wagonjwa,Wazee na Walemavu
Ni Vyema waandishi tukajenga Utayari wa kusaidia Jamii na ndizo zenye Uhitaji wa misaada muhimu na hata kihabari kuliko kujikita na wanasiasa kwa maslahi yao na wakati wao tu Muhimu Tujitambue tutetee haki zetu ikiwemo Kuajiriwa na kufungwa kwa mikataba kuliko ilivyo sasa zaidi ya asilimia 90 HATUJIELEWI
Sambamba na hilo Tujikite katika kuandika habari za Uchunguzi na fursa zipo kupitia TMF..Alimalizia Abdulaziz
Nae Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Lindi Bi Fortunata Kullaya ambae alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe hizo zilizokutanisha waandishi toka wilaya zote za mkoa wa Lindi aliwataka
Waandishi kuandika habari kwa kufuata maadili ili wasijiingize katika matatizo hasa katika kipindi hiki cha mchakato wa katiba na kuelekea katika uchaguzi mkuu hapo mwakani kwa kuwa wanahabari ni watu muhimu katika jamii pia aliwataka kufika vijijini kubaini baadhi ya changamoto ambapo pia aliwahakikishia kuwa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF sasa ndio mkombozi wa huduma za afya hivyo pelekeni Ujumbe Jamii
Ijiunge na ipate Tiba kwa Unafuu zaidi.
"Nyie ni wadau wakubwa wa NHIF, hivyo mbaini kuwa kalamu zenu zinaweza kujenga au kubomoa hivyo bima ya afya Tawi Lindi Tumeona ni siku muhimu sana kujumuika pamoja kwa kuwapima afya zenu ili mfanye kazi mkijijua".
Aidha katika maadhimisho hayo pamoja na kutoa msaada kwa Wagonjwa wa hospital ya Rufaa ya Sokoine na kupimwa kwa Afya za Waandishi kulifuatiwa na Tafrija Fupi ya Kutakiana heri iliyojumuisha waandishi na
wenza wao pamoja na wadau wengine wa habari iliyofanyika katika Fukwe za Santorin Beach Manispaa ya Lindi.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.