Unknown Unknown Author
Title: MENEJA WA WEMA SEPETU WATUPIANA VIJEMBE NA MPOKI JANA KWENYE TUZO ZA KILI, CHEKI HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Meneja wa Muigizaji maarufu wa Bongo Movie Wema sepetu amewaacha midomo wazi watu waliokuwa wamehudhuria Tuzo ya Muziki ya Kilimanjaro k...
Meneja wa Muigizaji maarufu wa Bongo Movie Wema sepetu amewaacha midomo wazi watu waliokuwa wamehudhuria Tuzo ya Muziki ya Kilimanjaro katika ukumbi wa mlimani City jana baada ya kupaniki na kujikuta anajibu mapigo kwa Mc wa sherehe hiyo Silvery Mjuni anayefahamika zaidi kwa jina la Mpoki.

Meneja wa Wema aitwae Martin Kadinda amejikuta ameshindwa kuzuia hisia zake kutokana na masihara ya mpoki pale alipowaambia kuwa timu Diamond ni kikundi kinachoongoza kupost picha hata zisizo na msingi kwenye mitandao ya kijamii hususani Instagram,

Mpoki aliwaambia  Diamond na wafuasi wake akiwemo wema,martin kadinda,Rommy Johnson kuwa  wanapost kila wakati kwa mfano wakiwawanakula,wamelala ndipo Martin kadinda alipomwambia mpoki kuwa atafute namna nyingine ya kutafutia pesa.

Kauli ya Kadinda iliwashangaza wengi kwani licha ya kuwa mpoki alikuwa anazungumza kimasihara lakini jambo lake linaukweli kwa kiasi kikubwa japo Kadinda alikuwa mwepesi kupanik na kushindwa kukubaliana na ukweli huo.


About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top