USAIN BOLT ALIZWA VIATU VYAKE JIJINI LONDON, SOMA HAPA

Usain bolt
Mwanariadha na bingwa wa medali ya dhahabu ya Olympic ya mbio fupi mjamaica Usain Bolt mapema wiki hii ametangaza kuibiwa viatu vyake vya kukimbilia. Viatu hivyo vyenye sahihi yake vina thamani ya £20,000 viliibiwa na mtu ambaye mpaka sasa hayajafahamika maeneo ya Croydon, jijini London.
viatu vya bolt

Baada ya kugundua wizi huo Bolt aliandika kwenye ukurasa wake wa tweeter....
"Najua unanipenda lakini kwanini umeiba viatu vyangu?, najua utavirudisha. Sawa? Ulipaswa kuja kuniomba hakuna sababu ya kuniibia"

Baada ya tukio hilo Bolt aliweka picha kwenye ukurasa wake wa tweeter ikimuonyesha akiweka sahihi kwenye viatu vyake vingine.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post