Unknown Unknown Author
Title: ANUSURIKA KIFO KWA KUCHOMWA KISU, MAPENZI YAHUSIKA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkazi mmoja wa Mkoani Mtwara amenusurika Kifo Baada ya Kuchomwa Kisu kifuani Mwake na wenzake katika ugomvi uliosababishwa na Kutofautiana...
Mkazi mmoja wa Mkoani Mtwara amenusurika Kifo Baada ya Kuchomwa Kisu kifuani Mwake na wenzake katika ugomvi uliosababishwa na Kutofautiana maneno kati ya Mjeruhiwa na wajeruhi huko eneo la Kiyanga.

Akisimulia jinsi Ilivyotokea Kijana huyu alisema ya kuwa aliombwa na msichana wake ampeleke kununua kiberiti na walipofika Kirabuni aliweza kuwasalimia watu waliokuwepo sehemu hiyo lakini Baadhi yao waliitikia na wengine Hawakuitikia na kuanza kutoa maneno mabaya Juu yake.

Baada ya Kuona hivyo aliweza kusimama na Kuwauliza kwanini wanamtolea maneno mabaya ilihali hajawakosea kitu chochote?, Ndipo Mmoja kati ya Wavulana waliokuwa wanatoa maneno hayo aliinuka na Kumrushia Ngumi na yule wa Pili pia aliinuka na Kumpiga Kifuani, Wakati huo hakuweza kujua kama Amechomwa Kisu kifuani kwani alikuwa katika harakati za Kukabiliana nao.

Baada ya Kuamuliwa na watu waliokuwepo katika eneo hilo ndipo walipoona kuwa amechomwa Kisu kifuani mwake na yeye mwenyewe alihisi mapigo ya Moyo Kubadilika.

Hivyo alikimbizwa Hospiali kwa ajili ya Matibabu ya haraka Na Hadi hivi sasa mtu huyo anaendelea Vizuri.

Msikilize hapa Akisimulia::

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top