Ryan Giggs Kocha wa Muda wa Manchester United
Kocha wa muda na mchezaji wa Manchester United Ryan Giggs 40 amesema hajui kama msimu ujao atakuwepo klabuni hapo.
Giggs ambaye amechukua nafasi ya kuwa kocha wa muda baada ya klabu hiyo Baada ya kumfukuza aliyekuwa kocha wake mkuu David Moyes wiki mbili zilizopita anaonekana kuwa na hofu na ujio wa kocha Louis Van Gaal.
Giggs amesema "Nitaondoka Manchester kama sitokuwa katika mipango ya kocha mpya ajaye, nia yangu ni kuendelea kuwa hapa kadri iwezekanavyo. Kocha akisema sikuhitaji kikosini ama kwenye benchi la ufundi nitachukua kila kilichochangu na kwenda kwingine kwa ajiri ya kuendelea na taaluma ya ukocha na siyo kucheza mpira."
Giggs pia amekiri kuwa na wiki moja ngumu sana amesema "Wiki hii nimekuwa na mambo mengi mno ikiwemo mipango ya ziara za klabu kwa ajiri ya maandalizi ya msimu mpya, kupitia mikataba ya wachezaji wetu wa kikosi cha pili waliopo klabuni pamoja na walioko nje kwa mkopo".
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.