BEN MWALALA ASIKITISHWA NA UZEMBE ULIOFANYWA NA KLABU YA YANGA, HII NI AIBU KUBWA

BEN Mwalala ametoa la moyoni na kutamka Mrundi Didier Kavumbagu na Frank Domayo hawakukosea kusaini Azam FC, lakini kinachomsikitisha ni kitendo cha Yanga kuzidiwa ujanja.

Mwalala mchezaji wa zamani wa Yanga na mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara 2008 amekiri kuwa yeye ni mpenzi wa klabu hiyo na anaongea ikiwa inamuuma moyoni.


Ameliambia Mwanaspoti kuwa: "Hata Ulaya katika klabu kubwa, wanapoona mchezaji ambaye wanamhitaji, tena ni kijana wanamsainisha mapema hata kama mkataba wake haujaisha kabisa. Anaweza kuwa amebakiwa na miezi mitatu au zaidi wao wanamwongeza ndiyo Yanga inatakiwa kuwa hivyo.”


“Unapomuongezea makataba ni faida kwa timu pia, kwani hata kama timu nyingine itakapokuwa inamuhitaji lazima mumuuze kwa pesa nyingi,” alisisitiza Mwalala ambaye ni Mkenya.


“Hiki ninachokiongea kinaniuma, ninaongelea Yanga na mimi ni Mwanayanga pia, inabidi tujipange, bila kuwa makini yanaweza kuibuka mengine mapya. Kwa ukubwa wa klabu ya Yanga, ndiyo inayotakiwa kuiba wachezaji, lakini siyo yenyewe iibiwe kama tukio hili lililotokea,” alisisitiza.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post