Unknown Unknown Author
Title: MG'AO WA KIM KARDASHIAN SIKU MOJA KABLA YA NDOA YAKE, WAITEKA MITAA YA PARIS UFARANSA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mg’ao wa Kim Kardashian siku moja kabla ya ndoa yake waiteka attention ya mitaa ya Paris Ufaransa.   Ingekuwa uswahilini kwetu tungekuw...
Kim Kardashian

Mg’ao wa Kim Kardashian siku moja kabla ya ndoa yake waiteka attention ya mitaa ya Paris Ufaransa. 

Ingekuwa uswahilini kwetu tungekuwa tunachambua mchele wa kesho tayari kwa ajili ya kula ‘ubwabwa’ wa mwali wetu dada Kim Kardashian, au leo usiku tungekesha kwenye vigodoro zinapigwa michiruki/minanda na sebene la taarabu… kunachimbika kwa shangwe (Naipenda Yanga/Simba Shabiki wa Damu). 

Lakini huko Paris Ufaransa, Kim Kardashian ameangusha party kubwa ya nguvu tangu jana ya kuuaga u-single (bachelorette Party), tayari kwa ajili ya kuwa Mrs Kanye West. Kim alifanya party akiwa na mama yake, mdogo wake Khole Kardashian na marafiki zake.

Jana usiku alienda club akiwa na marafiki zake kula bata la nguvu baada ya kumalizana na familia yake huku wote wakionekana wameng’aa ‘kisistaduuuh’.
Uwepo wa Kim Kardashian umeiteka attention ya mitaa ya Paris huku akifuatwa na paparazzi ambao wamekuwa wakipost kwenye mitandao wanayoifanyia kazi picha zinazomuonesha mrembo huyo akiwa ‘ametokelezea’.

Bwana Kanye West ambaye mara nyingi amekuwa katika ugomvi na paparazzi akipinga kupigwa picha, hivi sasa hawezi kukwepa picha kila anapoonekana ni ‘mwanga mithili ya uwepo wa manyunyu na radi’. 


So kesho ndio siku yenyewe..ambayo Kim K..atasema ‘I DO..I..I…DO’.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top