Unknown Unknown Author
Title: BAADA YA SIKU MOJA TU TANGU KUZIKWA KWA MAREHEMU KUAMBIANA YAMEANZA KUIBUKA MAPYA. SOMA HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MAMBO yameanza! Siku mbili tu baada ya mazishi ya mwigizaji na mwongoza filamu mahiri Bongo, marehemu Adam Kuambiana, mrembo mmoja ameibuka ...
MAMBO yameanza! Siku mbili tu baada ya mazishi ya mwigizaji na mwongoza filamu mahiri Bongo, marehemu Adam Kuambiana, mrembo mmoja ameibuka na kusema alikuwa mchumba wa marehemu, Ijumaa linakujuza.

Selina na Adam Kuambiana
Lulu Jumanne ‘Selina’, akiwa na marehemu Kuambiana.

Kwa mujibu wa mrembo huyo, Lulu Jumanne ‘Selina’, alifahamiana na marehemu Kuambiana mwaka 2006 akamwambia ndoa yake haipo sawasawa.
Alisema walianzisha uhusiano lakini haukuwa wazi katika jamii. Alisema siku moja akiwa anaishi Mwananyamala, wazazi wake walimtembelea.
“Nikiwa na wazazi nilimwona Kuambiana anapiga hodi, akaingia akiwa na begi la nguo. Niliogopa kwani wazazi walikuwepo na walikuwa hawamtambui.

SelinaMrembo anayejulikana kwa jina la Lulu Jumanne ‘Selina’.

“Hata hivyo, walielewa yakapita, tukawa tunaishi wote nyumbani kwa kupika na kupakua,” alisema Selina ambaye naye ni mwigizaji. Aliendelea kuweka wazi kwamba, baada ya hapo maisha yaliendelea lakini ikafika mahali marehemu akahamishia mapenzi kwa Mbongo Fleva, Stara Thomas yeye akawa ‘zilipendwa’.

Akizidi kuanika mambo kuwa mwaka jana Kuambiana alirudi kwake baada ya kutofautiana na Stara, akataka waendelee na mapenzi yao.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top