HAYA NDIO MAMBO YA SIRI NA YA NDANI ZAIDI USIYOJUA KUHUSU SHILOLE....CHEKI HAPA

Ni msanii mwenye ups and downs nyingi sana , kama unatafuta role model hapa bongo basi muite Shilole. Alianzia kwenye movie lakini kabla ya movie alishawahi kuuza chakula na biashara mbali mbali in order to survive.

Shilole katika pitapita zake kwa bahati mbaya alijikuta akilazishwa mapenzi wakati akiwa na umri mdogo sana, msanii huyo akiwa na miaka 14 tu alijikuta akiwa na mimba . “nilipata mimba nikiwa mdogo sana yani hata maziwa ndio yanaanza sipendi kitu hiki kimtokee msichana mwengine kwa kweli na pia kwa wale wanaume wenye tamaa plz wanapoteza future za watu” alisema  shilole.

Baada yakupata mtoto wake huyo, aliangaika nae na baadae alijikuta akiolewa na mtu mwingine na kuweza kupata mtoto wake wa pili akiwa na umri wa 18 na mwisho wa siku alitoka ndani ya ndoa na kuhamia Dar na kuanza maisha upya.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post