Unknown Unknown Author
Title: NAOMBA USHAURI:: ALINITAKA NITOE MIMBA SIKUTOA, SASA ANAMTAKA MTOTO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mimi ni msichana wa miaka 24, mwaka juzi nilipata ujauzito kutoka kwa aliyekuwa boyfriend wangu,ambaye nilikaa nae miezi 6. Lakini nilivyo...
Mimi ni msichana wa miaka 24, mwaka juzi nilipata ujauzito kutoka kwa aliyekuwa boyfriend wangu,ambaye nilikaa nae miezi 6. Lakini nilivyomwambia, akanambia yeye hayuko tayari kuwa na mtoto kwa sasa na akanishauri nitoe mimba hiyo. Mimi sikukubalina na hilo nikaamua kubeba mimba miezi 9, akaniacha na kukata mawasiliano na mimi kabisa. 

Nikajifungua mtoto wa kiume ambaye mpaka sasa ana mwaka mmoja na nusu. Sasa baba wa mtoto (yule aliyekuwa boyfriend wangu) anamtaka huyu mtoto amchukue na anasema sasa yuko tayari kumlea. Mimi bado nina hasira za yeye kunikataa kipindi kile wakati nina mimba na sitaki kabisa mawasiliano naye na mtoto sikumwandikisha jina lake kwenye cheti chake cha kuzaliwa. Anatishia kunipeleka mahakamani akidai mtoto wake.

Naombeni ushauri wenu nifanye nini, niko njia panda.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top