RAIS KASAINI SHERIA INAYORUHUSU WANAUME KUOA WANAWAKE WENGI

Familia ya mke zaidi ya mmoja ambapo kwa sasa Kenya Mwanaume ruksa kuoa wake wawili.

Nchini Kenya rais Uhuru Kenyatta ametia saini sheria inayowaruhusu wanaume kuoa wanawake wengi. Sheria hii ilionekana kupingwa vikali na wabunge wanawake hali iliyowafanya wasusie vikao vya bunge katika vikao kadhaa vilivyopita.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika ofisi ya Rais imesema, kuwa mswada huo ambao unaojumuisha vipengele kadhaa kuhusu ndoa , imekuwa sheria sasa. Mswada huo ulioleta mageuzi katika sheria ya sasa , ilipitishwa na bunge mwezi jana kuidhinisha rasmi utamaduni wa ndoa ya zaidi ya mwanamke mmoja.

Sheria hii kwa sasa bado inapata upinzani kutoka kwa shirikisho la kitaifa la mawakili wanawake pia limesema kuwa litapinga sheria hiyo mahakamani. Wabunge wote wanaume, na ambao ni wengi, waliunga mkono kuondolewa kwa kipengele katika sheria hiyo ya ndoa kilichomtaka mwanaume afanye mashauriano na mkewe kwanza kabla ya kuoa mwanamke mwingine.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post