MIKOSI YAMUANDAMA MCHEZAJI HUYU WA ARSENAL

Na. Paul Manjale
Kama kuna mchezaji mwenye bahati mbaya pengine kuliko wote duniani kwa sasa ni kiungo wa Arsenal mfaransa Abou Diaby.Diaby alirejea uwanjani jumanne ya wiki hii baada ya kuwa nje ya uwanja kwa miezi 13 katika mchezo uliovikutanisha vikosi vya U-21 vya Arsenal na Chelsea.Katika mchezo huo kikosi cha Arsenal kiliambulia kipigo cha bao 2-1 huku Diaby akipumzishwa dakika ya 45.Habari kutoka ndani ya kikosi cha Arsenal zinasema Diaby alipata majeraha kidogo hivyo hatokuwemo kwenye kikosi kitakachoivaa Newcastle jumatatu ya wiki ijayo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post