HONGERA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA KUUTUNZA NA KUULINDA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR KWA MIAKA 50


Lindi Yetu Blog inaungana na watanzania wote wapenda amani na utulivu kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya viongozi wake wakuu, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Piter Pinda pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Alli Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar , Maalim Seif Sharif Hamad, na Makamu wa pili wa Rais, Balozi, Seif Ali Idd kwa kuulinda na kutuongoza vyema wananchi wote katika kuulinda na kudumisha Muungano wetu kwa amani na Utulivu.

Pia tunawatakia kila la heri watanzania wote popote pale walipo kwa kusherehekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
"TUULINDE MUUNGANO WETU KWA MAENDELEO, AMANI NA USTAWI WA TAIFA LETU" na daima tukumbuke "UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU"

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post