HILI NI PIGO KWA TIMU YA CHELSEA, RAMIRES AFUNGIWA MECHI NNE ZA LIGI

RAMIRES AKIMCHEZEA NDIVYO SIVYO LARSSON

Na. Paul manjale
Klabu ya Chelsea imepata pigo katika mbio zake za kusaka ubingwa wa EPL baada ya kiungo wake mahiri raia wa Brazil Ramires kufungiwa michezo minne ya ligi na chama cha soka England FA.

FA imefikia hatua hiyo baada ya uchunguzi uliofanywa kupitia picha za Television kumuonyesha kiungo huyo akimfanyia madhambi mchezaji wa klabu ya Sunderland Sebastian Larsson katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa katika uwanja wa Stamford Blidge na Chelsea kulala kwa mabao 2-1.

Katika mchezo  huo uliofanyika jumamosi ya tarehe 19 mwamuzi wa kati Mike Dean hakuweza kuliona tukio hilo kutokana na umbali uliokuwepo kati yake na tukio lenyewe.

Ramires amekubaliana na adhabu hiyo hivyo atakosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Liverpool jumapili hii kisha mchezo dhidi ya Norwich City utakaofuatiwa na mchezo wa kufunga msimu wa ligi dhidi ya Cardiff City huku mchezo wa nne na wa mwisho katika adhabu hiyo utakuwa mwezi August katika msimu mpya wa 2014-2015.

Ikumbukwe adhabu ya kumfanyia madhambi Larsson ni michezo mitatu nje lakini FA imeongeza mmoja na kufikia minne kutokana na Ramires kutoka katika kifungo kingine kufuatia madhambi aliyofanya katika mchezo dhidi ya Aston Villa mwezi uliopita.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post