Younes Belhanda akipambana na wachezaji wa Arsenal
Na. Paul Manjale
Kiungo wa Dynamo Kiev Younes Belhanda(24) amefunguka kuwa ndoto na kiu yake ya
kucheza ligi kuu ya England bado iko pale pale.Belhanda akifanya mazungumzo na
gazeti la London 24 amesema ni hamu ya kila mchezaji kucheza hapo na kujifunza
mambo mengi nje na ndani ya uwanja.Belhanda ambaye ni mchezaji wa zamani wa
klabu ya Montpellier ameongeza kuwa akipata ofa toka England basi chaguo lake la
kwanza litakuwa ni kucheza katika klabu ya Arsenal kwa swahiba wake Olivier
Giroud waliyecheza wote Ufaransa na kuipa taji klabu ya Montpellier.
Tags
SPORTS NEWS
