FRANK LAMPARD BADO YUPO YUPO CHELSEA, KUSAINI MKATABA MPYA HIVI KARIBUNI

Frank Lampard
Na. Paul Manjale
Kiungo wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya England Frank Lampard 35 yuko mbioni kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja ili kubakia klabuni hapo.Hatua hiyo imefikiwa baada ya majadiliano ya muda mrefu baina ya pande hizo mbili kuonyesha kufurahishwa na namna mazungumzo yalivyokwenda.

Mkataba huo utasainiwa kabla ya kuisha mkataba wa sasa unaofikia ukingoni mwezi june, katika mkataba huo mpya Lampard atapokea mshahara unaokari biana na ule wa sasa wa £1,25000 kwa wiki,bonus pamoja na haki za matangazo.

Lampard ambaye msimu huu ameanza michezo 30 na kufunga magoli 8 amedumu na klabu hiyo kwa miaka 13 na kutwaa mataji kadhaa likiwemo taji la ligi ya mabingwa Ulaya amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia klabu ya LA Galaxy inayoshiriki ligi kuu ya Marekani.

Chanzo cha habari toka kambi ya Lampard kinasema "Frank anaipenda Chelsea na pia anapenda kucheza chini ya kocha Jose Mourinho hivyo akili yote ni kubaki Stamford Blidge"

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post