Vilanova alianza kusumbuliwa na maradhi hayo November 2011 na kufanyiwa operation ya kwanza New York Marekani..
Vilanova alichukua mikoba ya kuifundisha Barcelona msimu wa 2012/2013 kutoka kwa kocha Pep Guardiola na kuweka rekodi mpya klabuni hapo baada ya kushinda mechi 18 kati ya 19 za mwanzo wa msimu na kufanikiwa kutwaa taji la La Liga kwa pointi 100.
Vilanova alizaliwa mwaka 1968 huko kijijini Bellcaire d' Emporda,alijiunga na kituo cha soka cha Barcelona mwaka 1984 mpaka 1989 lakini hakuweza kupata nafasi kikosi cha kwanza. Badala yake alitimkia Celta Vigo na kisha Mallorca mpaka hapo soka yake ilipokuja kukatwishwa na majeraha ya goti.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi
Tags
SPORTS NEWS