Usiku wa Ijumaa ndani ya Makonde Royal Night Club Palikuwa hapatoshi kwani wanachuo wa T.I.A Mkoani Mtwara walifanya yao ndani ya Mjengo huo. Party hiyo Ilikuwa ya aina yake kwani ilikuwa na Events Nyingi nyingi kama Fasion show na Artist Performance.
Mzigo ulianza kwa Wasanii wa chuo hicho kupanda stejini Mmoja baada ya Mwingine.
Baadae sasa wale wazee wa Cartwalk walifanya yao Juu ya Jukwaa kwa kuonyesha Mavazi mbalimbali.
Hakika Walipendeza sana na Mavazi yao.
Baada ya Hapo Msanii ManSu Li a.k.a Underground King alihitimisha burudani kwa kupanda stejini na kutoa Bonge la Burudani kwa Wanachuo wenzake hao.
Sasa ilifika wakati wa Kudondosha Disco la Nguvu na ndio Suprise ilipotokea kwa kutokea Dj Mkali Mkoani Mtwara Mwite Ally Mchokoreka a.k.a Bwege na kutambulishwa rasmi kuwa Yuko ndani ya Mjengo huo Kuanzia siku hiyo na Kuendelea
So wale wapenzi wake wanaokunwa na Mikito yake wanaweza kupata burudani kupitia Mjengo huo kuanzia hivi sasa.
Na alidondosha bonge la Disco hadi Mishale ya Asubuhi.
Tags
HABARI ZA KITAIFA


















